Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
BAADHI ya wananchi na wawekezaji katika eneo la Zegereni, Manispaa ya Kibaha, Mkoa wa Pwani, wameiomba Serikali kujenga kwa kiwango cha lami barabara yenye urefu wa takribani kilometa mbili inayounganisha eneo hilo na viwanda, wakieleza kuwa hatua hiyo itakuwa suluhisho la kudumu la changamoto ya miundombinu, hasa wakati wa mvua.
Wamesema ujenzi wa barabara hiyo utaendana na kasi ya ukuaji wa shughuli za kiuchumi katika eneo hilo, ambalo limeendelea kuvutia uwekezaji wa viwanda na hivyo kuongeza mahitaji ya miundombinu bora ya usafirishaji.
Meneja wa Kinglion Investment Company, Kelvin Richard Boya, alisema ubovu wa barabara hiyo huathiri shughuli za uzalishaji, hususan wakati wa mvua, kutokana na magari makubwa kushindwa kupita kwa urahisi, hali inayochelewesha uingizaji wa malighafi na usafirishaji wa bidhaa.
Alisema hali hiyo wakati mwingine husababisha uzalishaji kusimama kwa muda na kuviingiza viwanda katika gharama na hasara zisizotarajiwa.
“Uzalishaji viwandani unapokwama kutokana na ubovu wa barabara, magari makubwa hushindwa kupita kufikisha malighafi au kusafirisha bidhaa zilizotengenezwa. Hali hii inasababisha viwanda kusitisha uzalishaji kwa muda na kupata hasara kubwa,” alisema Boya.
Kwa upande wake, dereva wa lori, Hamis Hassan, alisema madereva wa malori na magari ya makontena wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya magari kukwama kwenye matope wakati wa mvua, hali inayochelewesha mizigo kufika sokoni na kuongeza gharama za uendeshaji.
Akizungumza kwa niaba ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Kibaha, Colin Mwasheni, alisema barabara hiyo inayotambulika kama Zegereni Industry 5 ipo katika mpango wa kujengwa kwa kiwango cha lami ili kutoa huduma ya kudumu kwa shughuli za viwanda na wananchi wanaoitumia.
Mwasheni alisema kinachohitajika kwa sasa ni upatikanaji wa fedha ili kuwezesha kuanza kwa utekelezaji wa ujenzi huo.
Meya wa Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, alisema barabara hiyo ni muhimu kwa kuwa inahudumia viwanda tisa pamoja na wananchi, hivyo uboreshaji wake unaendana na azma ya kukuza uchumi kupitia uwekezaji na viwanda.
Alisema kuboresha miundombinu inayowaunganisha wawekezaji na masoko kutasaidia kuongeza uzalishaji, mapato na fursa za ajira.
Dkt. Mawazo alisema Manispaa ya Kibaha inaendelea kuweka mipango na mikakati ya kuboresha mazingira ya uwekezaji, ikiwa ni sehemu ya kwenda sambamba na juhudi za Serikali za kukuza sekta ya viwanda na uwekezaji nchini.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...