Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa (MCC), Salim Abri Asas, ametembelea wanafunzi wa Shule ya Msingi Weru, iliyopo katika jimbo la kalenga,wilaya ya Iringa Vijijini, na kupongeza mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi shuleni hapo.
Asas ameeleza kuridhishwa na mazingira hayo huku akitambua juhudi za Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kuboresha sekta ya elimu nchini.Amesema utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) unaendelea kuonekana kupitia maboresho ya miundombinu ya elimu na utoaji wa elimu bila malipo, hatua zinazolenga kuwawezesha wanafunzi kupata elimu katika mazingira bora.
Aidha, amewahimiza wanafunzi kusoma kwa bidii, kuzingatia nidhamu na kujituma katika masomo yao ili kunufaika na fursa za elimu na kupata matokeo mazuri katika mitihani.
Amisisitiza kuwa juhudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia zinapaswa kwenda sambamba na uwajibikaji wa wanafunzi, walimu na wazazi katika kuhakikisha elimu inayotolewa inaleta matokeo yanayotarajiwa.


.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...