Meneja Mkuu Mwandamizi wa Bolt Afrika Mashariki, Dimmy Kanyankole, aliwaalika madereva wa Bolt katika kifungua kinywa kilichofanyika katika ofisi za kampuni hiyo jijini Dar es Salaam, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja.
Katika hafla hiyo, Bolt imewazawadia madereva waliofanya vizuri na mafuta ya vyombo, matairi na zawadi nyingine mbalimbali ili kuwaunga mkono katika shughuli zao.
Kanyankole amewashukuru abiria na madereva kwa kuendelea kutumia huduma za Bolt, huku akiwahimiza kuzingatia sheria za usafiri na kuheshimiana katika kazi.
Aidha, kampuni hiyo imewahakikishia wateja kuwa inaendelea na jitihada za kuwezesha huduma za kupakia na kushusha abiria katikati ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa sasa, maeneo maalumu ya maegesho tayari yametengwa katika eneo la Feri, huku mipango ikiendelea ya kuanzisha maeneo mengine Posta na Kariakoo ili kurahisisha huduma za usafiri kwa abiria na madereva.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...