NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar, Ndugu Abdi Mahamoud Abdi, amesema CCM itaendelea kuisimamia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) ili kuhakikisha inatekeleza kwa ufanisi miradi mbalimbali ya maendeleo, hususan katika sekta ya elimu.

Ndugu Abdi ameyasema hayo baada ya kukabidhi vifaa vya ujenzi katika Skuli ya Maandalizi Kikaangoni, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa ziara yake ya kukagua uhai wa Chama kuanzia ngazi ya matawi ndani ya Jimbo la Mfenesini.

Amesema vifaa hivyo, vilivyotolewa kupitia Mfuko wa Jimbo la Mfenesini, vitasaidia kupunguza baadhi ya changamoto zinazoikabili skuli hiyo na kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia.

Vifaa vilivyokabidhiwa ni pamoja na gypsum board, ndoo za rangi na mbao, ambavyo vitatumika katika ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya skuli hiyo.

Amesisitiza kuwa CCM itaendelea kushirikiana na Serikali pamoja na wananchi katika kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa na inawanufaisha wananchi kwa wakati.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...