Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amezindua awamu ya pili ya bima ya afya kwa wote na kuwataka wananchi wa Mkoa huo kutumia fursa ya uwepo wa bima hiyo ya gharama nafuu ya shilingi lakimoja na nusu kwa familia ya watu sita ili kupata huduma bora za afya bila malipo ya papo kwa papo

Akizungumza leo Oktoba 22 Jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa bima ya afya kwa wote awamu ya pili Mkuu wa Mkoa Mhe Albert Chalamila amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kujiunga na bima hiyo ya afya ili kupata huduma bora za matibabu bila malipo ya papo hapo huku akisisitiza kuwa bima hiyo ni kwa ajili ua makundi yote bila kujali wenye kipato kidogo, kikubwa au wasio na kipato.

RC Chalamila amewataka wanawake wajawazito kutumia fursa ya uwepo wa bima hiyo ili kukabiliana na changamoto mbalimbali za kiafya wakati wa ujauzito licha ya kuwa Serikali inatoa huduma bure kwa wajawazito kwani uwepo wa bima hiyo itamuwezesha mama mjamzito kupata huduma kwenye ngazi mbalimbali za hospitali ikiwemo hospitali za rufaa za mikoa na ngazi zingine

Aidha RC Chalamila ametumia nafasi hiyo kuwataka wakuu wa Wilaya za mkoa huo kuendesha kampeni ya nyumba kwa nyumba ili kuhamasisha wananchi kujiunga na bima hiyo akieleza kuwa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu imeamua kuwapunguzia wananchi gharama za matibabu kwani kupitia bima hiyo familia ya watu sita itapata huduma za afya kwa gharama ya shililingi laki moja na nusu kwa mwaka mzima

Kwa upande wa Mkuu wa wilaya ya Ilala Mhe Edward Mpogolo akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya zote tano za mkoa huo wa Dar es Salaam amesema miongoni mwa malalamiko ya wananchi ni changamoto za upatikanaji wa huduma za afya hivyo bima hiyo inakwenda kumaliza changamoto hiyo

Naye Meneja wa mfuko wa bima ya afya kwa wote Mkoa wa Kinondoni Bw Fidelis Steven Shauritanga akizungumza kwa niaba ya mameneja wa mfuko huo kwa mikoa yote ya Dar es salaam ametaja huduma zinazopatikana kupitia bima hiyo kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo Kurenje Mbura Meneja kanda ya mashariki kutoka Mamlaka ya usimamizi wa bima TIRA amesema mamlaka hiyo itaendelea kusimamia vyema vigezo, ubora na sheria za huduma ya bima

Kupitia uzinduzi huo ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam umetoa ofa ya bima za afya kwa kaya kumi zenye uhitaji kupitia ofisi ya shekh wa Mkoa wa Dar es salaam, bima za kaya kumi kwa baba padre kutoka CCT aliyeongoza sala kwenye uzinduzi huo pamoja na bima za kaya kumi kwa chama cha mapinduzi Mkoa wa Dar es Salaam.












Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...