Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Mhe. Thomas Cornel Apson, amehitimisha ziara ya kutembelea tarafa nne za Wilaya ya Ikungi kwa lengo la kukutana na wanufaika pamoja na waombaji wa mikopo inayotolewa na Halmashauri kupitia asilimia 10 ya mapato ya ndani.
Katika ziara hiyo, Mhe. Apson aliambatana na viongozi wa Idara ya Maendeleo ya Jamii, ambapo alipata fursa ya kusikiliza maoni, changamoto na mapendekezo kutoka kwa wajasiriamali wa makundi mbalimbali, wakiwemo wanufaika na waombaji wa mikopo hiyo.
Ziara hiyo imelenga kubaini changamoto zinazowakabili walengwa katika upatikanaji na matumizi ya mikopo hiyo ili kuweka mikakati ya kuzitatua na kuboresha utekelezaji wa mpango huo kwa manufaa ya wananchi.
Akihitimisha ziara yake katika Tarafa ya Sepuka, Mkuu wa Wilaya aliahidi kushughulikia changamoto zilizobainishwa kwa kushirikiana na mamlaka husika, hatua inayolenga kuimarisha shughuli za ujasiriamali, kuongeza fursa za kiuchumi na kuboresha maisha ya wananchi wa Wilaya ya Ikungi.





Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...