Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amekutana na Rais wa AGRA, Bi. Alice Ruhweza, na kueleza hatua zinazochukuliwa na Tanzania kuimarisha kilimo na kuwawezesha vijana kushiriki katika sekta hiyo.

Mazungumzo hayo yamefanyika Oktoba 21, 2026, kando ya Mkutano wa Kimataifa wa Norman E. Borlaug (Borlaug Dialogue), jijini Des Moines, Jimbo la Iowa, Marekani. Waziri Mkuu anashiriki mkutano huo akimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dkt. Mwigulu amesema Serikali inaongeza uwekezaji katika umwagiliaji, uzalishaji wa mbegu bora, utafiti, huduma za ugani, maghala na miundombinu ya kuchakata mazao.

Aidha, amesema Tanzania inaendelea kushughulikia vikwazo vinavyowakabili vijana katika kilimo kwa kuwawezesha kupata ardhi, kuwapatia mafunzo na kuwaunganisha na benki ili kupata mitaji ya kununua mbegu, zana na pembejeo nyingine.











Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...