TANGA

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Jumatatu, Oktoba 5, 2026, anakuwa mgeni rasmi katika harambee ya kuchangia maendeleo ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki.

Harambee hiyo inafanyika katika Viwanja vya Tanga Beach Resort, jijini Tanga, ikiwa na lengo la kuhamasisha waumini na wadau mbalimbali kuchangia uimarishaji wa huduma na miradi ya maendeleo ya Dayosisi hiyo.

Miongoni mwa maeneo yanayolengwa kuimarishwa kupitia harambee hiyo ni vituo vya huduma pamoja na shughuli za diakonia zinazolenga kuwahudumia na kuwasaidia watu wenye mahitaji mbalimbali katika jamii.
















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...