Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Ndg. Shomari Mndolwa, akifungua semina ya kuwajengea uelewa kuhusu majukumu yanayotekelezwa na EWURA, Watendaji Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji leo 30 Septemba mjini Nzega

Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Karim Ally akitoa elimu kuhusu majukumu ya EWURA kwa Watendaji na Viongozi wa Serikali za Mitaa wa Halmashauri ya Mji wa Nzega wakati wa semina iliyofanyika leo tar 30 Septemba 2026


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Ndg. Shomari Mndolwa, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua semina ya kuwajengea uelewa kuhusu majukumu yanayotekelezwa na EWURA, Watendaji Kata, Mitaa na Wenyeviti wa Mitaa na Vijiji leo 30 Septemba mjini Nzega

Na.Mwandishi Wetu-Nzega

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) Kanda ya Magharibi, imekutana na Watendaji Kata na Mitaa pamoja na Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Vijiji wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, leo tarehe 30 Septemba 2026 kwa lengo la kuwapa elimu kuhusu udhibiti wa huduma za nishati na maji.

Akifungua semina hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Nzega, Ndg. Shomari Mndolwa, ameishauri EWURA kuendelea kuweka mifumo imara ya udhibiti inayozingatia na kulinda maslahi ya watoa huduma na walaji huku ikitoa huduma za udhibiti zinazolenga kutekeleza Dira ya Taifa ya 2050.

Meneja wa EWURA Kanda ya Magharibi, Mha. Karim Ally, ameeleza kuwa viongozi wa serikali za mitaa ni daraja na nguzo muhimu katika utekelezaji wa shughuli za kiudhibiti zinazohusisha utaoaji wa leseni, vibali na utatuzi wa malalamiko kati ya watoa huduma na wateja.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...