Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, katika Maonesho ya Tisa ya Kitaifa ya Teknolojia ya Madini yanayoendelea Viwanja vya Dk. Samia Suluhu Hassan mkoani Geita.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TISEZA, Absalom Kibanda, alisema mbele ya waandishi wa habari Oktoba 1, 2026 kuwa mamlaka hiyo inaendelea kuweka mazingira rafiki yatakayowawezesha wawekezaji kuitumia fursa hiyo na kuongeza mchango wa madini kwenye uchumi wa Taifa.
Kwa mujibu wa Kibanda, sekta ya madini ni miongoni mwa maeneo yenye uwezo mkubwa wa kuchangia malengo ya maendeleo ya nchi, huku ukuaji wake ukionekana wazi zaidi mkoani Geita.
Naye Meneja wa Kanda ya Ziwa wa TISEZA, Venance Mashiba, alibainisha kuwa mamlaka hiyo inawagusa wawekezaji wote bila ubaguzi, wakubwa na wadogo, kwa msingi kuwa kila kundi lina nafasi katika kukuza uchumi.
Mashiba alieleza kuwa TISEZA inashirikiana na taasisi zenye utaalamu wa masuala ya madini katika kuwapatia wawekezaji taarifa na kuwaelekeza maeneo yenye uhakika wa uwepo wa madini.
Aliongeza kuwa kuimarisha ushirikiano huo kutasaidia kuongeza ufanisi wa kuvutia uwekezaji, kupunguza changamoto zinazowakabili wawekezaji na kuhakikisha fursa zilizopo zinanufaisha Taifa kwa ujumla.



.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...