Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini ambaye ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Judith Kapinga amekabidhi kilo 1,000 za mbegu za kahawa kwa AMCOS 20 na kikundi kimoja ili kuzalisha vitalu vya miche ya kahawa ili kuweza kuzalisha miche milioni 3.5 na kuendeleza jitihada za kuzalisha kahawa Wilayani humo.

Amekabidhi mbegu hizo  Oktoba 07,2026 wakati wa Ziara yake alipotembelea Halmashauri ya Mbinga iliyopo katika Jimbo hilo ambapo amesema  amesema uchumi wa Halmashauri hiyo ni kilimo cha kahawa kwani msimu uliopita halmashauri hiyo imezalisha tani elfu 18 na kwa msimu huu imepanga kuzalisha tani 19 ambapo mpaka sasa imevuka malengo hayo  kabla ya msimu kuisha.

Waziri Kapinga ameongeza kuwa utoaji wa mbegu hizo ni kuchagiza uzalishaji wa kahawa kwa wingi ili kuchochea uchumi kwa wananchi wa Mbinga pamoja na upatikanaji wa mapato kwa halmashauri.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...