KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Kenani Kihongosi, amekagua ujenzi wa jengo la kitegauchumi la chama hicho katika Kata ya Utete, Wilaya ya Rufiji, mkoani Pwani.
Jengo hilo linajengwa kwa gharama ya Sh bilioni mbili na linatarajiwa kuwa na ofisi za jumuiya zote tatu za CCM, ambazo ni Umoja wa Wazazi, Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT).
Aidha, jengo hilo litakuwa na maduka pamoja na ukumbi wa mikutano, miundombinu inayolenga kuimarisha shughuli za chama na kuongeza fursa za mapato kupitia matumizi ya jengo hilo.
Mradi huo unatarajiwa kuhudumia zaidi ya watu 2,000, ukiwa sehemu ya juhudi za kuimarisha miundombinu ya CCM, kuboresha mazingira ya utendaji wa jumuiya zake na kukuza shughuli za kiuchumi wilayani Rufiji.
Ujenzi huo pia unalenga kuweka mazingira bora ya utekelezaji wa majukumu ya chama pamoja na shughuli za kibiashara zinazotarajiwa kunufaisha wanachama na wananchi wa wilaya hiyo.
Katika ziara hiyo, Kihongosi aliambatana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Pwani, Mwinshehe Mlao, Mbunge wa Jimbo la Rufiji ambaye pia ni Waziri wa Afya, Mohamed Omary Mchengerwa, pamoja na viongozi wengine wa chama.


.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...