Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na Kamati ya Wataalamu ya Maandalizi ya Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), wamefanya ukaguzi wa mwisho wa maandalizi ya mkutano huo unaotarajiwa kufanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano Arusha (AICC).
Ukaguzi huo umefanyika leo, Oktoba 2, 2026, ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa AICC, Bi. Christine Mwakatobe, ambapo viongozi hao walikagua miundombinu na maeneo mbalimbali muhimu yatakayotumika wakati wa mkutano huo.
Miongoni mwa maeneo yaliyokaguliwa ni ukumbi mkuu wa mikutano, kumbi za vikao vya pembeni, ofisi za viongozi, mifumo ya sauti na tafsiri, eneo la waandishi wa habari pamoja na maeneo ya mapokezi ya wageni.
Baada ya ukaguzi huo, Makatibu Wakuu wameiagiza Kamati ya Kitaifa ya Maandalizi kukamilisha maboresho na marekebisho ya mwisho katika maeneo ambayo bado yanaendelea kufanyiwa kazi, kabla ya kuanza kwa mkutano huo.
Mkutano wa 153 wa IPU unatarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 4 hadi 9, 2026, na kuhudhuriwa na washiriki takribani 2,000 kutoka mabunge 183 wanachama wa IPU.
Washiriki hao wanatarajiwa kujumuisha Maspika, Wabunge, Makatibu wa Mabunge pamoja na maafisa mbalimbali kutoka nchi wanachama.
Mkutano huo unatarajiwa kuwa fursa muhimu kwa Tanzania kuonesha uwezo wake katika kuandaa mikutano mikubwa ya kimataifa, pamoja na kukuza diplomasia ya kibunge, utalii na fursa mbalimbali za kiuchumi.

.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...