Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
TIMU ya watoa huduma wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili katika Manispaa ya Kibaha, imewataka wanafunzi wa Kata ya Visiga kutofumbia macho vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa, badala yake watoe taarifa kwa walimu, wazazi, polisi kupitia Dawati la Jinsia na Watoto pamoja na viongozi wa mitaa ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa.
Elimu hiyo inalenga kuhakikisha kuwa shule zinakuwa sehemu salama, ambapo kila mwanafunzi anafahamu haki zake, anajua mahali pa kupata msaada anapofanyiwa ukatili na anaweza kuendelea na masomo pamoja na kutimiza ndoto zake bila hofu.
Wito huo umetolewa timu hiyo ikiongozwa na Adv. Revocatus Thadeo Mathew, wakati timu hiyo ilipotembelea Shule ya Msingi Visiga na Shule ya Sekondari Visiga, kwa ajili ya kutoa elimu ya kisheria kwa wanafunzi kuhusu haki zao, kujitambua na namna ya kujilinda dhidi ya vitendo vya ukatili.
Ofisa maendeleo Manispaa ya Kibaha Anitha Kashaija amesisitiza umuhimu wa wanafunzi kujua haki zao na kutambua vitendo vya unyanyasaji, akiwataka kuwa na ujasiri wa kutoa taarifa mapema ili hatua stahiki zichukuliwe na kuhakikisha wanapata mazingira salama ya kujifunzia.
Amesema elimu hiyo inalenga kuwajengea wanafunzi uelewa wa kisheria tangu wakiwa wadogo, ikiwemo kutambua haki zao za kikatiba na kisheria, umuhimu wa kuwa na vyeti vya kuzaliwa pamoja na kujua sehemu wanazoweza kupata msaada wanapokabiliwa na changamoto zinazohatarisha usalama wao.
Katika ziara hiyo, Revocatus ameeleza timu hiyo pia ilitoa elimu na huduma za kisheria kwa wananchi wa Kata ya Visiga, Manispaa ya Kibaha, kuhusu masuala mbalimbali ikiwemo haki za wananchi, ukatili wa kijinsia na migogoro ya ardhi.
Wananchi walipata fursa ya kushiriki mkutano na watoa huduma hao, kuwasilisha changamoto zinazowakabili na kupata ufafanuzi pamoja na mwongozo wa kisheria kuhusu masuala mbalimbali yaliyowasilishwa.
Ziara hiyo ni sehemu ya mwendelezo wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria katika kata mbalimbali za Manispaa ya Kibaha kupitia Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Awamu ya Pili, inayolenga kuwawezesha wananchi kufahamu haki zao na kupata msaada wa kisheria katika kutatua changamoto zinazowakabili.

.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...