Na Mwandishi wetu, Mirerani
CHAMA cha wachimbaji madini Mkoa wa Manyara (MAREMA) kimeiomba Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, lango la kuingilia na kutoka ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite mji mdogo wa Mirerani kuwa wazi saa 24 ili wachimbaji wafanye kazi zao usiku na mchana.
Mwenyekiti wa MAREMA, Elisha Nelson Mnyawi ameeleza hayo mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti wake Subira Mgalu ilipofanya ziara yake ya kutembelea machimbo ya madini ya Tanzanite.
Elisha amesema wachimbaji madini ya Tanzanite ni wachapakazi, waaminifu na waadilifu hivyo wapewe muda wa saa 24 ili wafanye kazi ya kuchimba madini kwa ufanisi.
"Hapa ndani ya ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite tuna vyombo vyote vya ulinzi na usalama, hivyo tunaomba lango la kuingilia na kutokea liwe wazi saa 24 ili tufanye kazi," amesema Elisha.
Ameeleza kuwa japokuwa lango hilo hufungwa saa 5 usiku ila mchimbaji haruhusiwi kuingiza chochote inapofika saa 12 jioni hivyo kukwamisha uchimbaji wa usiku.
"Unakuta mchimbaji amefanikiwa kupata zana za kufanyia kazi mgodini saa 12 jioni ila haruhusiwi kuingiza kwenye lango hilo hivyo tunaomba lango liwe wazi saa 24 na vyombo vya ulinzi na usalama wapewe zamu ya kulinda mchana na usiku," amesema.
"Pia wachimbaji wana changamoto ya kulipia ankara kubwa ya nishati ya umeme kupitia kituo walichoweka kiitwacho KVA kwani kinawatesa wachimbaji," amesema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa MAREMA Tawi la Mirerani, Samwel Rugemalila amesema taarifa potofu za wachimbaji madini ya Tanzanite kutorosha madini zinapaswa kupuuzwa.
"Wachimbaji wanafanya kazi yao wakipata uzalishaji wanalipa kodi ya Serikali na kuendelea na mambo yao hii zana ya utoroshaji kwa wachimbaji haipo," amesema Rugemalila.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge Subira Mgalu ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo amewapongeza wachimbaji madini ya Tanzanite na kuahidi kukutana na wadau wa madini jijini Dodoma ili kupeana mrejesho.
Mgalu amesema baada ya kusikiliza changamoto za wachimbaji watakaa hivi karibuni na Wizara ya Madini jijini Dodoma ili kujadili hayo kwa lengo la kuboresha uchimbaji.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...