Na Janeth Raphael - MichuziTv Bungeni
Mbunge wa Jimbo la Katavi, Thomas Kampala Maganga, ameitaka Serikali kueleza mikakati na hatua inazochukua kukabiliana na mmomonyoko wa maadili katika jamii, akitaja vitendo vya ushoga kuwa miongoni mwa changamoto zinazohitaji kushughulikiwa.
Akizungumza leo, Oktoba 30, 2026, bungeni jijini Dodoma, Mbunge huyo amesema pamoja na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali kudhibiti hali hiyo, bado kuna ongezeko la vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili katika jamii.
Kutokana na hali hiyo, ameitaka Serikali kuweka wazi mikakati zaidi itakayotumika kukabiliana na changamoto hiyo, pamoja na namna itakavyoshirikisha jamii katika kulinda misingi ya maadili.
Akijibu hoja hiyo, Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Maryprisca Mahundi, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na viongozi wa mitaa, vijiji na kata pamoja na maafisa maendeleo ya jamii kuimarisha malezi na kukabiliana na changamoto za mmomonyoko wa maadili, hususan miongoni mwa vijana.
Amesema utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa kukabiliana na mmomonyoko wa maadili umeanza, huku akisisitiza kuwa mafanikio ya juhudi hizo yanahitaji ushirikiano wa karibu kati ya Serikali na wananchi.
Mahundi amebainisha kuwa jukumu la kulinda maadili si la Serikali pekee, bali linapaswa kuwa la jamii nzima kwa kusimamia mila, desturi na tamaduni zinazojenga malezi bora. Aidha, amewataka wazazi kutimiza wajibu wao kwa kuwapa watoto muda wa kutosha, kuzungumza nao mara kwa mara na kufuatilia mwenendo wao, badala ya kujikita katika shughuli za kutafuta kipato na kusahau malezi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...