Na Victor Masangu, Kibaha
MSTAHIKI Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Mawazo Nicas, ametoa siku saba kwa kiwanda cha kuchakata plastiki cha Cordy, kilichopo Kata ya Picha ya Ndege, kuhakikisha kinaweka mfumo sahihi wa majitaka na kuacha kutiririsha maji machafu katika maeneo ya makazi ya wananchi.
Dkt. Nicas ametoa agizo hilo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kiwanda hicho na kubaini kuwa bado kinaendelea kutiririsha maji machafu katika maeneo yanayozunguka makazi ya wananchi, licha ya kupewa maelekezo mara kadhaa na viongozi mbalimbali.
Ziara hiyo imefanyika kufuatia malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi wa Mtaa wa Picha ya Ndege kuhusu harufu kali pamoja na maji yenye rangi nyeusi yanayotiririka mitaani na kuingia katika makazi yao.
Wananchi wamedai kuwa hali hiyo imekuwa ikisababisha athari mbalimbali kwa jamii na viumbe hai, ikiwemo mifugo kufa baada ya kunywa maji hayo.
Akiwa katika eneo hilo, Dkt. Nicas akiwa na timu kutoka Idara ya Mazingira ya Manispaa, alibaini kuwepo kwa bomba pamoja na chemba iliyokuwa imeelekezwa moja kwa moja kwenye mtaro unaopita katika maeneo ya makazi ya wananchi.
Dkt. Nicas amesema Manispaa hiyo imewahi kufika katika kiwanda hicho na kutoa maelekezo ya kukomesha tatizo hilo, lakini utekelezaji wake haujawa wa kuridhisha.
Amesema kiwanda hicho hakina mfumo wa kutibu na kuchuja maji taka kabla ya kuyatoa nje ya kiwanda, huku pia kikiwa hakina kibali kutoka mamlaka husika ya Bonde la Maji kwa ajili ya kutiririsha maji.
“Tumeshafika hapa mara ya kwanza na kutoa maelekezo, lakini wamekuwa wakaidi. Hili ni jambo hatari kwa afya ya jamii,” amesema Dkt. Nicas.
Ameagiza kiwanda hicho ndani ya siku saba kujenga mfumo wa kutibu maji taka kabla ya kuyatiririsha, huku mamlaka ya bonde ikitakiwa kufanya taratibu za ukaguzi na utoaji wa kibali baada ya maji hayo kutibiwa kwa mujibu wa taratibu.
Aidha, Dkt. Nicas ametoa muda hadi Jumapili, Oktoba 12, 2026, kwa kiwanda hicho kuhakikisha kinavisafisha vyanzo na mtaro unaopokea maji hayo machafu.
Amesema atarejea katika eneo hilo kukagua utekelezaji wa maagizo hayo na kwamba iwapo hayatatekelezwa, Manispaa itachukua hatua kwa mujibu wa sheria.
Kwa upande wake, Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Bryson Mpogoza, amesema kiwanda hicho kiliwahi kutozwa faini na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), baada ya kubainika kutotekeleza matakwa ya kimazingira.
Amesema kiwanda hicho kiliahidi kutekeleza maelekezo yaliyotolewa, lakini ukaguzi wa hivi karibuni umebaini kuwa baadhi ya changamoto bado zinaendelea.
Dkt. Nicas amesema Manispaa itaendelea kusimamia utekelezaji wa maagizo hayo, ikiwemo kuhakikisha maeneo yaliyoathiriwa na majitaka yanasafishwa na mfumo sahihi wa uchujaji na utibaji wa maji taka unajengwa.
Katika ziara hiyo, Meya pia alitembelea Kiwanda cha Keds na kukipongeza kwa hatua kilizochukua katika kupanua mtaro kwa urefu wa takribani mita 600.
Amekitaka kiwanda hicho kuendelea kushirikiana na jamii na kuongeza urefu wa mtaro huo ili kusaidia kupunguza changamoto ya maji katika eneo hilo.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wa Mtaa wa Picha ya Ndege wamemshukuru Meya kwa kufika katika eneo hilo na kusikiliza malalamiko yao.
Wananchi hao pia wameeleza wasiwasi kuhusu madai ya kuwepo kwa kemikali katika eneo la Kiwanda cha Lake Oil, hasa wakati wa mvua.
Akizungumzia suala hilo, msimamizi wa kiwanda hicho ambacho bado kiko katika hatua za ujenzi, amesema kwa sasa hakuna kemikali zinazomwagwa katika eneo hilo, bali mabaki yaliyopo ni ya awali.
Dkt. Nicas amemwagiza msimamizi huyo kuhakikisha magari yanatumika kuondoa udongo unaodaiwa kuwa na mabaki ya kemikali na kuweka mchanga mpya, ili kupunguza hatari kwa mazingira na jamii inayozunguka eneo hilo.

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...