Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), mdhamini mkuu wa Ligi Kuu ya NBC, imeongeza msisimko katika Dabi ya Kariakoo kati ya Simba SC na Yanga SC kwa kuandaa shughuli mbalimbali zilizowakutanisha mashabiki wa soka na wateja wa benki hiyo, huku ikimkabidhi mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu, tuzo ya mchezaji bora wa mechi hiyo.

Simba SC iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga SC, katika mchezo uliovuta hisia za mashabiki wa soka na kuongeza msisimko wa ushindani kati ya miamba hiyo ya soka nchini.

Kupitia shughuli hizo, NBC ilitumia fursa ya mchezo huo mkubwa kuimarisha uhusiano na wateja wake huku ikiendeleza dhamira yake ya kuunganisha huduma za kibenki na uzoefu wa kipekee kwa wadau wa michezo.

Kabla ya mchezo huo, benki hiyo iliwawezesha baadhi ya wateja wake kusafiri kwa msafara maalumu kuelekea Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambako walishuhudia pambano hilo kutoka jukwaa la VIP, wakipata fursa ya kufurahia dabi hiyo katika mazingira ya kipekee.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa NBC, Elibariki Masuke, aliongoza shughuli hizo na kumkabidhi Elie Mpanzu tuzo ya mchezaji bora wa mechi, katika tukio lililoshuhudiwa na mashabiki waliokuwa uwanjani na watazamaji waliofuatilia matangazo ya moja kwa moja kupitia televisheni.

Sambamba na shughuli za uwanjani, maofisa wa NBC walitoa huduma mbalimbali za kibenki kwa mashabiki na wadau waliohudhuria mchezo huo, zikiwemo huduma za kufungua akaunti na ushauri wa kifedha. Hatua hiyo ilitoa fursa kwa benki hiyo kuwasogezea wateja huduma zake, huku ikiendeleza ushiriki wake katika kukuza mchezo wa soka nchini.

Akizungumza kuhusu ushiriki wa NBC katika dabi hiyo, Masuke alisema kuwa benki hiyo inaendelea kutumia michezo mikubwa kuimarisha uhusiano na wateja wake pamoja na wadau wengine wa soka.

“Udhamini wetu hauishii tu katika kuboresha ligi tunazodhamini, bali pia katika kuhakikisha kuwa wadau wetu, wakiwemo wafanyakazi, viongozi na wateja, wanakuwa sehemu ya moja kwa moja ya mchezo huu. Tunataka soka liwe uzoefu wa kipekee, si tukio la dakika 90 pekee,” alisema Masuke.

Aliongeza kuwa NBC inaendelea kubuni mikakati ya kuboresha Ligi Kuu ya NBC kwa lengo la kukuza vipaji, kuongeza ushindani, kuchochea ajira kupitia michezo na kuimarisha hamasa ya soka nchini.

Katika misimu ya hivi karibuni, NBC imeendelea kuunga mkono maendeleo ya soka kupitia udhamini wa ligi na shughuli mbalimbali zinazolenga kuimarisha mazingira ya ushindani na ustawi wa mchezo wa miguu. Miongoni mwa maeneo ya ushiriki wake ni kuwezesha upatikanaji wa huduma za kifedha, zikiwemo bima ya afya na mikopo ya usafiri kwa timu, pamoja na kusaidia hafla za utoaji wa vikombe na tuzo.

Kupitia udhamini huo, NBC imekuwa ikiunganisha michezo, huduma za kifedha na ushirikiano na wateja, huku ikiimarisha nafasi yake kama mdau wa maendeleo ya soka na michezo nchini Tanzania.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa NBC, Elibariki Masuke (kulia) akimkabidhi tuzo mshambuliaji wa Simba, Elie Mpanzu (kushoto) alieibuka mchezaji bora kwenye mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyowakutanisha Simba SC dhidi ya Yanga SC maarufu kama ‘Kariakoo Derby’ iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam. Pambano hilo lilimalizika kwa timu ya Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Yanga SC.

Mkurugenzi wa Wateja Wadogo wa NBC, Elibariki Masuke (kulia) na Mkuu wa Kitengo cha Mikakati wa Benki NBC, Msafiri Shayo (kushoto) wakifuatilia mchezo huo

Kikosi cha Simba kilichovaana na Yanga jana

Kikosi cha Yanga kilichovaana na Simba jana


Wachezaji wa Simba na Yanga wakishangilia magoli yao yaliyofungwa kwa nyakati tofauti.


Baadhi ya washabiki wa Simba na Yanga wakishangilia wakati wa mchezo huo.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...