Na Janeth Raphael - MichuziTv
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempongeza mtangulizi wake, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli, kwa kusimamia na kuendeleza utekelezaji wa mpango wa kuhamishia makao makuu ya Serikali jijini Dodoma, akisema hatua hiyo imekuwa sehemu muhimu ya kutimiza ndoto ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ya kuwa na makao makuu ya nchi katikati ya Tanzania.
Amesema mafanikio yaliyofikiwa katika kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya Serikali ni matokeo ya maono na juhudi za viongozi mbalimbali waliotangulia, hivyo ni muhimu kwa Watanzania kutambua na kuthamini mchango wao katika safari hiyo ya kihistoria.
Rais Samia ameyasema hayo wakati akizindua Mji wa Serikali wa Mtumba jijini Dodoma, mradi mkubwa wa kimkakati uliojengwa kwa gharama ya zaidi ya Shilingi Bilioni 700, ukiwa na majengo ya ofisi za wizara na taasisi mbalimbali za Serikali pamoja na miundombinu wezeshi.
Amesisitiza kuwa hatua ya kuhamishia shughuli za Serikali Dodoma ilikuwa na lengo la kusogeza huduma karibu zaidi na wananchi, kurahisisha upatikanaji wa huduma za umma na kupunguza gharama ambazo wananchi walilazimika kuzitumia kufuata huduma hizo katika maeneo mbalimbali.
Hata hivyo, Rais Samia amebainisha kuwa kuhamia kwa makao makuu ya Serikali Dodoma hakumaanishi kuwa wananchi wote wanapaswa kusafiri hadi jijini humo ili kupata huduma za Serikali, akieleza kuwa Serikali inaendelea kuimarisha matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika utoaji wa huduma.
Amesema matumizi ya mifumo ya kidijitali yanaendelea kupanuliwa ili kuwawezesha wananchi kupata huduma za Serikali wakiwa katika maeneo yao, bila kulazimika kufika Dodoma, hatua inayolenga kupunguza usumbufu, muda na gharama za wananchi.
Uzinduzi wa Mji wa Serikali wa Mtumba unaweka hatua nyingine muhimu katika safari ya kuimarisha Dodoma kama kitovu cha shughuli za Serikali, huku ukiakisi mwendelezo wa maono yaliyoasisiwa na viongozi waliotangulia na kuendelezwa na Serikali zilizofuata kwa manufaa ya Taifa.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...