Dar es Salaam iliwaka wakati vijana wenye vipaji mbalimbali walipokutana katika usaili wa Serengeti Lite Nyota Bigi Msimu wa Pili, wakipewa nafasi ya kuonyesha uwezo wao na kung’arisha vipaji walivyonavyo.

Usaili huo umeleta pamoja vijana wenye vipaji vya kuimba, kucheza, kuigiza, kuchekesha, wanamitindo na ubunifu mwingine mbalimbali, na kuwaleta kwenye jukwaa moja ili waonyeshe kile wanachoweza kufanya mbele ya watazamaji na wataalamu wa tasnia.

Kupitia ushirikiano na KUNTA Africa, Serengeti Lite inaendelea kutoa nafasi kwa vijana kuamini vipaji vyao, kuvitumia na kufikiria zaidi kupitia kaulimbiu “Lite Your Imagination.”

Baada ya Dar es Salaam, safari ya kutafuta Nyota Bigi inaendelea Arusha, Dodoma na Mwanza, ambapo vijana wengine watapata nafasi ya kuonyesha vipaji vyao na kuwania nafasi ya kuwa Nyota Bigi wa msimu huu.

Nani ataibuka kuwa Nyota Bigi? Safari bado inaendelea.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...