Na Mwamvua Mwinyi, Bagamoyo
SERIKALI imewahakikishia wananchi wanaodai fidia baada ya kupisha maeneo kwa ajili ya ujenzi wa Bandari ya Mbegani Bagamoyo, mkoani Pwani, kuwa inaendelea kuchukua hatua kuhakikisha wanalipwa stahiki zao huku taratibu za malipo zikiendelea.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, ametoa kauli hiyo wakati wa ziara ya kukagua utekelezaji wa mradi huo, ambapo amewataka wananchi kuwa na utulivu na kuendelea kuunga mkono ujenzi wa bandari hiyo inayolenga kuwa kituo cha kimkakati cha kuhudumia shehena zinazoingia na kutoka nchini.
Amesema utekelezaji wa Bandari ya Mbegani pamoja na uboreshaji wa Bandari Ndogo ya Bagamoyo utachochea shughuli za kiuchumi, kuongeza fursa za ajira kwa vijana wa Wilaya ya Bagamoyo na kuongeza mapato ya Serikali.
Kwa mujibu wa Nyongo, bandari hiyo pia inalenga kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam, ambayo inakabiliwa na ongezeko la shehena na mahitaji ya kuhudumia meli kubwa za kisasa.
Amesema Bandari ya Mbegani itakuwa kituo mbadala kitakachosaidia kuongeza uwezo wa kuhudumia shehena, kupunguza muda wa meli kusubiri nangani na kurahisisha usafirishaji wa mizigo ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wake, Mbunge wa Bagamoyo, Subira Mgalu, amesema wananchi wamepata matumaini kutokana na uamuzi wa Serikali chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kuanza utekelezaji wa ujenzi wa Bandari ya Mbegani pamoja na maboresho ya Bandari Ndogo ya Bagamoyo.
Mgalu amesema ushirikishwaji wa wananchi katika mradi huo unaonekana, huku akieleza kuwa wana imani Serikali itahakikisha wananchi waliopisha maeneo ya mradi wanalipwa fidia zao.
“Licha ya wananchi kuahidiwa kulipwa fidia, pia walipewa ahadi ya kupewa maeneo, hivyo hili Serikali iliangalie kwa umuhimu wake,” amesisitiza Mgalu.
Naye Mkurugenzi wa Bagamoyo SEZ, Felix Michael, amesema tathmini iliyofanyika imebaini kuwa jumla ya watu 1,154 wamelipwa fidia, huku watu 4,005.3 ambao tathmini yao ilifanyika miaka 16 iliyopita bado hawajalipwa.
Amesema pia watu 1,130 hawajafanyiwa tathmini, hali inayofanya jumla ya watu 5,135 kuwa bado hawajalipwa fidia au hawajafanyiwa tathmini.
Kwa upande wake, Mhandisi Stephen John Mbogella, akimwakilisha Mkurugenzi wa Bandari, amesema Serikali imekamilisha uthamini na utwaaji wa eneo lote la mradi lenye ukubwa wa hekta 887.
Amesema kati ya eneo hilo, hekta 407 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya bandari, huku hekta 480 zikitengwa kwa ajili ya maeneo ya lojistiki na usafirishaji.
Mbogella amesema jumla ya Sh49,007,851,429.84 zimeshalipwa kama fidia kwa wananchi waliopisha maeneo kwa ajili ya mradi huo.
Amesema kwa sasa mchakato wa ununuzi unaendelea kwa ajili ya kumpata mkandarasi atakayetekeleza kazi ya kuchimba na kuongeza kina cha lango kuu la kuingilia meli pamoja na eneo la kugeuzia meli.
Kwa mujibu wa Mbogella, utekelezaji wa mradi huo umegawanywa katika awamu tatu, ambapo awamu ya kwanza itahusisha ujenzi wa magati matatu yenye uwezo wa kuhudumia makasha 1,012,500 (TEUs) kwa mwaka, sawa na shehena yenye uzito wa tani 23,287,500.
Ameeleza kuwa kiasi cha shehena kinachohudumiwa nchini kimefikia zaidi ya tani milioni 30 mwaka 2026 na kinatarajiwa kufikia zaidi ya tani milioni 50 ifikapo mwaka 2030.
Amesema ongezeko hilo linahitaji uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu mipya na imara ya bandari ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya usafirishaji wa mizigo nchini.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...