NA Janeth Raphael - MichuziTv
Wakati maandalizi ya uzinduzi wa Mji wa Serikali Mtumba yakifikia hatua za mwisho, waendesha bodaboda, wamefanya ziara katika baadhi ya majengo ya serikali kwa lengo la kufahamu huduma zitakazopatikana na namna zitakavyoweza kuwasaidia katika shughuli zao za kila siku.
Ziara hiyo iliyofanyika leo, Oktoba 29, 2026, jijini Dodoma, imefanyika siku moja kabla ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuzindua majengo ya serikali pamoja na barabara za lami zilizojengwa katika eneo hilo.
Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Bodaboda, Guta na Bajaji Tanzania, Saidi Kagomba, amesema wameamua kutembelea mji huo mapema ili kupata maelezo kutoka kwa wataalamu kuhusu majukumu ya taasisi mbalimbali na huduma ambazo wananchi wanaweza kuzifuata. Amesema ziara hiyo inalenga kuwapa uelewa mpana kabla ya uzinduzi rasmi wa mradi huo mkubwa wa serikali.
Kagomba amesema wamepanga kutembelea majengo matano yanayohusiana na mahitaji yao, yakiwamo Wizara ya Maji, Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara inayoshughulikia masuala ya vijana, Ofisi ya Rais-TAMISEMI na Wizara ya Uchukuzi. Ameeleza kuwa Wizara ya Maji ni muhimu kwao kwa kuwa maji ni hitaji la msingi katika maisha ya kila siku, huku akitarajia kupata ufafanuzi kutoka TAMISEMI kuhusu uwezekano wa kuboresha vituo vya bodaboda na bajaji ili viwe vya kisasa na vikidhi mahitaji ya watoa huduma hao.
Aidha, amesema wanataka kufahamu taratibu za kisheria zinazohusu shughuli zao za usafirishaji, ikiwamo upatikanaji wa leseni kupitia taasisi husika, pamoja na namna wanavyoweza kupata msaada wa serikali wanapokabiliwa na changamoto zinazohitaji uingiliaji wa mamlaka za umma. Kwa mujibu wa Kagomba, kuwafahamu wahusika na majukumu ya kila taasisi kutawasaidia kujua mahali sahihi pa kupeleka mahitaji na changamoto zao.
Akizungumza na kundi hilo, Fred Kaduma kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Watu Wenye Ulemavu, amesema Mji wa Serikali Mtumba umejengwa kwa ajili ya kurahisisha shughuli za kiutawala na kutoa mazingira ya huduma kwa viongozi, watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla.
Amesisitiza kuwa majengo hayo si kwa matumizi ya viongozi na watumishi pekee, bali wananchi wanapaswa kufahamu uwepo wake na huduma wanazoweza kupata. Kwa upande wake, Paul Frank Nyongo kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu ameeleza historia ya mradi huo, hatua zilizofikiwa na maandalizi ya uzinduzi, akisema ziara hiyo inatoa fursa kwa wananchi kuelewa zaidi namna mji huo ulivyopangwa na shughuli zitakazofanyika ndani yake.
Ziara hiyo imeongeza uelewa wa wadau wa usafirishaji kuhusu umuhimu wa Mji wa Serikali Mtumba, ambao unalenga kukusanya ofisi za serikali katika eneo moja ili kurahisisha uratibu na kuboresha utendaji.

.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...