Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) limemchagua Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Mussa Azzan Zungu, kuwa Rais wa Mkutano wa 153 wa Umoja huo unaoendelea jijini Arusha.

Hoja ya kumchagua Mhe. Zungu kuwa Rais wa Mkutano huo ilitolewa na Spika wa Bunge la Wawakilishi la Uingereza (House of Commons), Sir Lindsay Hoyle, na kuungwa mkono na wawakilishi kutoka Uganda na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).

Uchaguzi huo umefanyika wakati wa Kikao cha Baraza la Uongozi la Umoja wa Mabunge Duniani kinachofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha (AICC).



















Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...