Na Said Mwishehe,Michuzi TV
TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wabunge Wanawake kwa mwaka 2026 wa Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu.
Akizungumza leo Oktoba 31,2026 jijini Dar es Salaam Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu amesema mkutano huo muhimu unatarajiwa kuwa na washiriki zaidi ya 300 kutoka nchi 12 za Ukanda wa Maziwa Makuu na unatarajia kuanza Novemba 2 mwaka katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa Julius Nyerere.
“Na utawakutanisha viongozi wakuu na wadau mbalimbali ili kujadili masuala yenye maslahi ya pamoja katika kukuza maendeleo, amani, na ushirikiano wa kikanda. Mgeni rasmi katika ufumguzi wa mkutano huo ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Viongozi wengine mashuhuri watakaohudhuria hafla ya ufunguzi ni pamoja na Judith Suminwa Tuluka ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ambaye ni mgeni maalum; Adao Francisco Correia de Almeida ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Angola naRais wa Jukwaa la Kibunge la Nchi za Ukanda wa Maziwa Makuu;
“Wengine ni Amason Jeffah Kingi ambaye ni Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Jacob Oboth – Oboth ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Uganda, Aime Boji Sangara ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zubeir Ali Maulid ambaye ni Spika wa Baraza la Wawakilishi la Zanzibar na Malungo Chisangano ambaye ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Zambia.”
Zungu amesema mkutano huo unafanyika chini ya kauli mbiu isemayo ‘Amani na maendeleo kwa ajili ya Ukanda wa Maziwa Makuu.Lengo lake kuu ni kuimarisha ushirikiano na kuongeza mchango wa wanawake katika maamuzi, Diplomasia ya kibunge, amani, usalama na maendeleo endelevu kwenye Ukanda wa Maziwa makuu.
Aidha, Mkutano huo ni fursa muhimu ya kuimarisha mshikamano na ushirikiano miongoni mwa nchi wanachama, pamoja na kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto zinazoukabili ukanda wetu.
Vilevile, amesema Tanzania kuwa Mwenyeji wa Mkutano huo kunaleta taswira chanya kwa nchi yetu kuendelea kuaminiwa na mataifa mengine kama nchi yenye amani na inayoendeleza na kutambua misingi ya utawala bora chini ya Uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan.
Ametoa mwito kwa Watanzania wote kushirikiana kwa pamoja ili kuhakikisha wageni wanapokelewa kwa bashasha, upendo, na ukarimu uleule unaoitambulisha nchi yetu duniani. Hiyo ni fursa adhimu ya kuwaonesha utamaduni wetu tajiri, mshikamano wetu thabiti, na uzuri wa kipekee wa Tanzania yetu.
“Kila mmoja wetu na awe balozi mwema kwa kuonesha heshima, nidhamu ya hali ya juu, usafi wa mazingira yetu, na moyo wa dhati wa kuwajali wageni wetu. Wewe ukiwa kama Mtanzania simama kama balozi, ili kila mgeni atakayeondoka, aondoke na kumbukumbu nzuri na zisizosahaulika mioyoni mwao kuhusu Tanzania.”

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...