Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira Tanzania (TRAMEPRO) limetoa wito kwa Watanzania kuendelea kuenzi misingi ya umoja, amani, upendo, uadilifu na uzalendo iliyoachwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Wito huo umetolewa katika ujumbe maalumu wa kumbukizi ya miaka 27 tangu kifo cha Mwalimu Nyerere, ambapo shirika hilo limeungana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Watanzania wote kumuenzi kiongozi huyo aliyekuwa nguzo muhimu katika kujenga misingi ya taifa.

TRAMEPRO limehimiza vijana, viongozi wa dini na vyombo vya habari kuendeleza maadili mema, mshikamano na uwajibikaji katika jamii, huku likisisitiza umuhimu wa kulinda afya za wananchi, kutunza mazingira na kuendeleza matumizi salama ya dawa asilia.

Shirika hilo limeeleza kuwa kumuenzi Mwalimu Nyerere hakupaswi kuishia katika kumbukizi pekee, bali kunapaswa kuonekana kupitia matendo yanayochochea maendeleo, haki, amani na ustawi wa Watanzania.

TRAMEPRO limetoa ujumbe huo jijini Dar es Salaam, Oktoba 14, 2026, likisisitiza kuwa misingi iliyoachwa na Baba wa Taifa inaendelea kuwa muhimu katika kujenga Tanzania yenye umoja, maadili na maendeleo endelevu.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...