Na Victor Masangu, Pwani

WAZIRI wa Katiba na Sheria, Abdallah Ulega, amewaagiza wataalamu wanaoshiriki Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia awamu ya pili kutekeleza majukumu yao kwa weledi na kuhakikisha wananchi wote wanapata haki bila ubaguzi, hususan wenye uwezo mdogo kiuchumi na makundi ya wanyonge.

Ulega ametoa agizo hilo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia awamu ya pili katika Mkoa wa Pwani, uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya Maili Moja, Wilaya ya Kibaha.

Uzinduzi huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi (CCM), wabunge, wawakilishi wa taasisi mbalimbali pamoja na wananchi.

Amesema ni muhimu kwa wataalamu hao kuhakikisha wananchi wanapata huduma za kisheria kwa mujibu wa sheria na taratibu za nchi, ili kuwawezesha kutatua changamoto zinazowakabili na kupata haki zao.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, amesema kampeni hiyo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa maeneo ya pembezoni ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakikabiliwa na changamoto mbalimbali za kisheria, hususan migogoro ya ardhi.

Amesema huduma hizo za bure zitasaidia kuwawezesha wananchi, hasa wanawake na watoto, kupata msaada wa kisheria na kutatua changamoto zinazowakabili.

Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Edwin Swale, amempongeza Rais wa Awamu ya Sita, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuanzisha kampeni hiyo inayolenga kuwasaidia wananchi kupata haki zao.

Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia awamu ya pili inalenga kuwafikia wananchi na kuwapatia huduma za kisheria bila malipo katika masuala mbalimbali, yakiwemo migogoro ya ardhi, mirathi, ukatili wa kijinsia na utatuzi wa changamoto nyingine za kisheria.




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...