Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mshindi kutoka Malawi Paul Chidale, tuzo baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom Tanzania Open 2026 jijini Arusha, Chidale alimaliza mashindano hayo kwa mikwaju 289 na kujinyakulia Sh9.35 milioni, akifuatiwa na Mtanzania Nuru Mollel aliyeshika nafasi ya pili kwa mikwaju 293 na Robinson Owiti kutoka Kenya aliyemaliza wa tatu kwa mikwaju 294.


Rais wa chama cha Golf nchini (Tanzania Golf Union - TGU) Gilman Kasiga, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mchango wa Vodacom Tanzania Open katika kukuza ushindani na kuendeleza mchezo wa golf nchini, wakati wa mashindano hayo yaliyofanyika Kili Golf Course jijini Arusha, Oktoba 22 hadi 25, 2026. Mashindano hayo yaliwakutanisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi mbalimbali wakishindania zawadi za jumla ya Sh40 milioni.

Mkuu wa Idara ya Masoko na Uwezeshaji wa Vodacom Tanzania Plc, Joseph Sayi, akishiriki mchezo wa gofu wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha. Katika mashindano hayo, mchezaji kutoka Malawi, Paul Chidale, aliibuka mshindi na kujinyakulia Sh9.35 milioni baada ya kumaliza kwa mikwaju 289, akiwashinda Nuru Mollel wa Tanzania na Robinson Owiti wa Kenya.

Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (kulia) akimkabidhi mchezaji golf kutoka Malawi, Paul Chidale, mfano wa hundi ya Sh9.35 milioni baada ya kutwaa ubingwa wa Vodacom Tanzania Open 2026 jijini Arusha. Chidale alimaliza mashindano hayo ya siku nne kwa jumla ya mikwaju 289, akimzidi Mtanzania Nuru Mollel aliyeshika nafasi ya pili kwa mikwaju 293 na Robinson Owiti kutoka Kenya aliyemaliza nafasi ya tatu kwa mikwaju 294.

Baadhi ya washiriki na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania Plc wakiwa kwenye mazoezi wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha katika viwanja vya Kili Golf Club jijini Arusha. Mashindano hayo ya siku nne yaliwakutanisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi nyingine mbalimbali, wakishindania zawadi za jumla ya Sh40 milioni.




Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando, akishiriki mchezo wa gofu wakati wa mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika katika viwanja vya Kili Golf Club jijini Arusha, Oktoba 22–25, 2026. Mashindano hayo yaliofanyika kwa siku nne yaliwakutanisha wachezaji wa gofu kutoka Tanzania na nchi nyingine, huku jumla ya zawadi za Sh40 milioni zikitolewa kwa washindi.




Baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania PLC na wadau mbalimbali, wakiongozwa na Mkurugenzi wa Vodacom Business, Nguvu Kamando (wa nne kulia), wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kilele cha mashindano ya Vodacom Tanzania Open 2026 yaliyofanyika jijini Arusha. Mashindano hayo yaliwashirikisha wachezaji kutoka Tanzania na nchi nyingine, yakiwa sehemu ya mchango wa Vodacom katika kukuza mchezo wa gofu, kuendeleza vipaji na kuimarisha ushindani wa mchezo wa gofu nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...