-Ni baada ya kufanyika maboresho yanayowezesha kubeba taarifa zote za mwananchi
-Sasa hadi kundi lako la damu,namba ya mlipa kodi zote zitapatikana ndani ya NIDA
Na Said Mwishehe,Michuzi TV-Kibaha
WANANCHI wanaotarajia kufunga ndoa nchini watalazimika kutumia Kitambulisho cha Taifa (NIDA) kuthibitisha utambulisho wao, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kuunganisha mifumo ya usajili na utambuzi wa watu na taasisi mbalimbali za Serikali.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), James Kaji, wakati akielezea maboresho ya kitambulisho kipya cha taifa, akisema Serikali inalenga kujenga mfumo mmoja wa kidijitali utakaounganisha taarifa muhimu za mwananchi kuanzia kuzaliwa hadi kufariki.
Amesema NIDA inaendelea na mazungumzo na taasisi mbalimbali, ikiwemo viongozi wa dini, ili kuunganisha mifumo yao na mamlaka hiyo, hatua itakayowezesha taarifa za ndoa, vyeti vya kuzaliwa na talaka kuthibitishwa kupitia utambulisho mmoja.
Ameongeza mfumo huo pia utasaidia kudhibiti matumizi ya vitambulisho vya watu wengine, ikiwemo wageni wanaotumia utambulisho wa Watanzania kupata huduma ambazo hawastahili.
Akizungumza leo Novemba 18,2025 katika uzinduzi wa kitambulisho kipya cha taifa na teknolojia mpya ya uzalishaji wake, Kaji amesema kitambulisho hicho kimeboreshwa kutoka kuwa nyenzo ya kumtambua mtu pekee na kuwa nyenzo pana ya kurahisisha upatikanaji wa huduma mbalimbali.
“Tutazungumza na viongozi wetu wa dini watumie vitambulisho vya NIDA katika kufungisha ndoa. Bila kuwa na kitambulisho cha NIDA hakuna ndoa, kuna watu sio raia wanakuja wanachukua dada zetu,wanachukua kaka zetu na kufunga ndoa kumbe wana mambo yao,hivyo kupitia kitmbulisho cha NIDA kutakuwa na taarifa zote ,hata kukiwa na talaka kitaonesha.”
Kaji amesema kupitia kitambulisho cha kipya cha NIDA kitakuwa na uwezo wa kuunganisha taarifa na huduma muhimu, zikiwemo za cheti cha kuzaliwa, bima ya afya, namba ya mlipa kodi (TIN) na kundi la damu, huku mazungumzo yakiendelea na taasisi husika ili kuwezesha matumizi hayo.
Ameongeza kwa upande wa bima ya afya, baadhi ya mifumo tayari imeanza kutumia utambulisho wa NIDA, hivyo mwananchi ataweza kupata huduma bila kulazimika kubeba kitambulisho kingine cha bima.
Kuhusu kundi la damu, amesema pia taarifa hiyo itawekwa kwenye kitambulisho ili kurahisisha utambuzi wa awali wakati wa dharura, ikiwemo ajali, ingawa wahudumu wa afya wataendelea kufanya vipimo vya kuthibitisha kabla ya kutoa huduma.
Aidha, amesema kitambulisho hicho kitakuwa na uwezo wa kutumika kama hati ya kusafiria katika baadhi ya nchi za Afrika Mashariki na Kati ambazo zimekubaliana na Tanzania, kupitia mfumo wa utambuzi unaounganishwa na mamlaka za uhamiaji.
Ameongeza maboresho hayo yamefanyika katika maeneo matatu makuu ambayo ni usalama, uimara na uwezo wa matumizi, huku teknolojia ya Laser Engraving ikitumika kuchora taarifa na picha za mwananchi ndani ya tabaka la kadi badala ya kuchapisha wino juu ya uso wake.
Alieleza kuwa teknolojia hiyo inalenga kuondoa changamoto ya vitambulisho kufutika, iliyokuwa ikilalamikiwa na wananchi katika mfumo wa zamani, pamoja na kupunguza uwezekano wa kughushi.
Pia kitambulisho kipya pia kina vipengele vya kisasa vya usalama, ikiwemo alama zinazobadilika kulingana na mwanga, vinavyotambulika kwa mguso, pamoja na teknolojia ya QR Code na Machine Readable Zone (MRZ) kwa ajili ya kusoma na kuthibitisha taarifa za mwananchi.
Katika hatua nyingine, amesema NIDA imepata msukumo mkubwa wa uwekezaji kutoka kwa Rais Samia Suluhu Hassan, ikiwemo kuongezewa bajeti na vitendea kazi vilivyosaidia kuboresha utoaji wa huduma.
Kuhusu vitambulisho vya zamani, Kaji amesema vile vilivyokuwa vikifutika kutokana na changamoto za teknolojia ya awali vinaweza kurejeshwa katika ofisi za NIDA kwa ajili ya kubadilishwa bila malipo.
Pia amesema mamlaka hiyo ina zaidi ya vitambulisho milioni 1.2 ambavyo havijachukuliwa na wahusika, hivyo kuwataka wananchi kuvifuata ndani ya miezi mitatu kuanzia Novemba 19, 2026, kabla ya kusitisha matumizi ya namba zilizotolewa kwa waliosajiliwa lakini hawajachukua vitambulisho vyao.
“Maboresho hayo ni sehemu ya safari ya kuijenga Tanzania ya kidijitali, ambako utambulisho mmoja utawezesha taasisi mbalimbali kuthibitisha taarifa za wananchi na kutoa huduma kwa urahisi, usalama na ufanisi zaidi.”

.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...