Na Mwandishi Wetu, Simanjiro
DIWANI wa Kata ya Naberera, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara, Marco Munga, ameiomba Serikali kuchukua hatua za haraka kudhibiti tembo wanaovamia makazi ya wananchi na kusababisha vifo.
Munga ametoa ombi hilo katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro kilichofanyika makao makuu ya wilaya hiyo, Orkesumet, akieleza kuwa matukio ya tembo kuvamia makazi yamesababisha hofu na taharuki miongoni mwa wananchi.
Amesema wiki iliyopita, kijana mwenye umri wa miaka 16 aliuawa na tembo katika eneo hilo, hali inayohitaji hatua za haraka za kukabiliana na wanyama hao.
“Wiki iliyopita kuna kijana mdogo wa miaka 16 ameuawa na tembo, jambo lililosababisha hofu kwa wakazi wa eneo hilo. Tunaomba hatua zichukuliwe ili kudhibiti tembo hao,” amesema Munga.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Kaleya Melita Mollel, ametoa pole kwa wananchi wa Naberera na maeneo mengine ya wilaya hiyo walioathiriwa na matukio ya tembo.
Mollel amemtaka Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kushirikiana na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) kuandaa mpango mkakati wa kudhibiti wanyama hao.
Aidha, amesisitiza umuhimu wa kufuatilia utaratibu wa kulipa fidia kwa wananchi walioathiriwa na matukio hayo ili kuhakikisha wanapata stahiki zao.
Naye, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo, Gracian Max Makota, amesema Halmashauri imeweka mikakati kwa kushirikiana na TAWA kukabiliana na changamoto hiyo.
Amesema mikakati hiyo inahusisha kutoa elimu kwa jamii kupitia mikutano ya vitongoji, vijiji na nyumba za ibada, pamoja na kuwafundisha wananchi mbinu na kuwapatia zana za kujikinga na tembo.
Makota ameongeza kuwa vituo vya kukabiliana na wanyama waharibifu vinaendelea kujengwa, ambapo kituo kimoja kinajengwa katika Kijiji cha Kandasikira na kingine kinatarajiwa kujengwa Naberera.
Kwa upande wake, Afisa Wanyamapori wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Aloyce Olodonjilalo, amesema kikosi cha doria kinaendelea na msako wa tembo hao ili kudhibiti vitisho vinavyowakabili wananchi.
Olodonjilalo amesema TAWA imepatia eneo hilo ndege mmoja aina ya ndege nyuki kwa ajili ya kusaidia kuwafukuza na kuwahamisha tembo.
Ameongeza kuwa idadi ya askari imeongezwa baada ya kupatiwa mafunzo, huku baadhi yao wakipelekwa katika Chuo cha Wanyamapori cha Sekamaganga, Tabora, kwa ajili ya mafunzo zaidi.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...