Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu (SBUU), Dkt. Jim Yonazi, akiwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. James Kilabuko, amekutana na ujumbe wa viongozi kutoka Kampuni ya KYM na Yonsei University Consortium ya nchini Korea, kwa ajili ya kujadili mapendekezo ya Kampuni hiyo ya kuanzisha Kituo cha Afya katika Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma.

Kituo hicho kinachopendekezwa kuanzishwa kwa ufadhili wa Serikali ya Korea, kinalenga kutoa huduma za afya kwa Watumishi wa Umma wanaofanya kazi katika Mji wa Serikali Mtumba.

Uanzishwaji wa kituo hicho unatarajiwa kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa watumishi ndani ya eneo la Mji wa Serikali, kupunguza changamoto za kufuata huduma hizo maeneo mengine, pamoja na kuboresha mazingira ya kazi na huduma za kijamii katika mji huo.

Hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za kuendeleza Mji wa Serikali Mtumba kuwa eneo lenye miundombinu na huduma muhimu zinazokidhi mahitaji ya Watumishi wa Umma.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...