Na Mwandishi Wetu

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo 25 Novemba 2026 imetoa elimu kwa madereva bajaji, magari yanayotumia gesi asilia iliyokandamizwa (CNG) na umma kwa ujumla kuhusu kanuni za usalama, katika eneo la kituo cha CNG cha TPDC, Sam Nujoma Dar es Salaam.

Madereva hao, pamoja na mambo mengine wamekumbushwa kuvifanyia ukaguzi vyombo vyao vya usafiri kwa kuzingatia utaratibu, kuhakikisha hakuna mivujo ya gesi na kutoweka mizigo juu ya mtungi wa CNG kwani inaweza kusababisha uharibifu.

Aidha, EWURA imetumia fursa hiyo kupokea mrejesho kuhusu huduma za CNG katika vituo ambapo madereva wameeleza kuwa, kwa ujumla hali ya utoaji huduma ni ya kuridhisha isipokuwa wapo baadhi ya wahudumu wenye kauli ziziso za staha,hivyo kuiomba EWURA kufuatilia na kuchukua hatua stahiki.

Vilevile, wameitaka EWURA kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika vituo vya CNG ili kupanua wigo wa huduma hususan kuanzia Ubungo hadi Kibamba ambapo hakuna kituo kwa sasa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...