Mbunge wa Ileje ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi Eng. Godfrey Kasekenya ametoa pole kwa familia zilizoathiriwa na moto ulioteketeza msitu Wilayani Ileje.

Mbunge huyo amewataka wananchi hao kuendelea kuwasaidia waathirika wa moto huo kupata hifadhi na matibabu wakati  juhudi za Serikali kuwasaidia kupata misaada zaidi zikiendelea.

Akiwa jimboni Ileje Eng. Kasekenya ametoa misaada mbalimbali ikiwemo fedha za matibabu kwa baadhi ya waathirika wa moto huo na kuhimiza jamii kusaidiana wakati wote.

Moto huo ambao unadaiwa kuzuka  Oktoba 23, 2026 Wilayani humo umeteketeza mashamba ya miti ya wananchi katika Vijiji vya  Chilemba, Lali, Shikunga na Ibaba ambapo wananchi hao wameiomba Serikali kupata msaada wa miche ya miti ili kupanda upya mvua zitakapoanza.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...