Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi, amefanya ziara ya kikazi katika Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), ambapo amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Makao Makuu ya taasisi hiyo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita katika kuendeleza sekta ya uhifadhi na utalii, ambapo utafiti ni nguzo muhimu.
Dkt. Abbasi ameipongeza TAWIRI kwa mchango wake mkubwa katika kufanya tafiti zenye tija katika uhifadhi na utalii, pamoja na kuimarisha ustawi wa jamii, hususan kupitia tafiti zinazosaidia kudhibiti migongano kati ya binadamu na wanyamapori.
"Hakikisheni tafiti mnazofanya zinawafikia wananchi kwa lugha inayoeleweka," amehimiza Dkt. Abbasi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI, Dkt. Eblate Mjingo, ameishukuru Serikali kwa uwekezaji katika ujenzi wa jengo hilo la kisasa la ghorofa tatu, na kuahidi kuendelea kusambaza matokeo ya tafiti kwa wadau wakiwemo wananchi.




.jpeg)




Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...