NA DENIS MLOWE, IRINGA
MKUU wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, amesema majeruhi wa ajali ya basi la Maokoto iliyotokea katika eneo la Masumbo, barabara kuu ya Iringa–Mbeya, wanaendelea vizuri na huduma za matibabu huku Serikali ikiahidi kuendelea kuhakikisha wanapata matibabu hadi watakapopona.
Kheri ameyasema hayo baada ya kuwatembelea majeruhi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa, ambapo alipata nafasi ya kujionea hali zao na maendeleo ya matibabu wanayoendelea kupatiwa na kuwapatia fedha za matunda na kujikimu wakati wakiendelea na matibabu.
Amesema mkoa umepata pigo kubwa kutokana na ajali hiyo iliyosababisha vifo vya watu na wengine kujeruhiwa, huku akieleza kuwa juhudi za kuokoa maisha ya majeruhi na kuhakikisha wanapata huduma stahiki zinaendelea.
Amesema hali za majeruhi waliolazwa hospitalini hapo zinaendelea vizuri, jambo linaloonesha kuwa huduma zinazotolewa na wataalamu wa afya zinasaidia kurejesha afya zao ili waweze kurejea katika majukumu yao ya kila siku.
“Serikali imedhamiria kuhakikisha wagonjwa wote ambao bado wanaendelea na matibabu wanapata huduma zinazostahili hadi watakapopona na kurejea katika shughuli zao za kawaida,” amesema Kheri.
Aidha, amewapongeza madaktari, wauguzi, manesi na wasimamizi wa sekta ya afya mkoani humo kwa namna walivyojipanga kuwapokea na kuwahudumia majeruhi tangu walipopata taarifa za ajali hiyo.
Amesema hakuna mgonjwa aliyepoteza maisha kutokana na uzembe wa wahudumu wa afya, akieleza kuwa majeruhi wote waliopokelewa wameendelea kupatiwa huduma kwa wakati na kwa kuzingatia mahitaji yao ya kiafya.
Amesisitiza kuwa Serikali itaendelea kufuatilia hali za majeruhi hadi watakapopata nafuu, huku wale watakaoruhusiwa kurejea nyumbani wakiendelea kufuatiliwa kuhakikisha wanaimarika kiafya.
Pia amewataka madaktari na wahudumu wengine wa afya kuendelea kushirikiana na familia za majeruhi kwa kutoa taarifa za maendeleo ya matibabu katika kila hatua ili ndugu waweze kufahamu kinachoendelea katika vituo vya afya vinavyowahudumia wapendwa wao.
Katika hatua nyingine, Kheri ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao katika ajali hiyo, akieleza kuwa ni msiba mkubwa ambao utachukua muda kusahaulika.
Amesema viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali wataungana na familia zilizofikwa na msiba huo katika kipindi hiki cha maombolezo na shughuli za mazishi, huku akiwataka wananchi kuendelea kuonesha mshikamano na kuwafariji waliofiwa.
Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Wanawake na Uzazi, Scholastica Malangalila, ambaye ni kaimu nafasi ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, amesema hospitali hiyo ilipokea majeruhi watano wa ajali hiyo, wakiwemo mwanaume mmoja na wanawake wanne.
Amesema tangu walipopokelewa, hospitali ilijipanga kutoa huduma kulingana na mahitaji ya kila mgonjwa na kwamba hadi wakati akizungumza, majeruhi wote watano walikuwa wakiendelea vizuri.
Ameeleza kuwa kwa mujibu wa tathmini ya madaktari, wanatarajia majeruhi hao kurejea katika hali zao za kawaida baada ya siku tatu, iwapo maendeleo ya matibabu yataendelea kuwa mazuri.
Kuhusu miili ya watu waliofariki katika ajali hiyo, Malangalila amesema hospitali imeendelea kutoa huduma kwa ndugu waliofika kuitambua na kuchukua miili ya wapendwa wao, huku akibainisha kuwa zoezi hilo lilikuwa likiendelea bila changamoto yoyote.

.jpg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...