Na Victor Masangu, Pwani

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, amesema lengo kuu la Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni kuwahudumia wananchi na kushirikiana na viongozi katika kuwaletea maendeleo.

Amesema hayo wakati wa hafla ya kujitambulisha rasmi kwa viongozi wa CCM na Serikali mkoani Pwani, kufuatia kuteuliwa kwake kuwa mlezi mpya wa chama hicho mkoani humo.

Amesema atashirikiana na viongozi na wanachama wa CCM katika Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kuhakikisha chama kinaendelea kujengwa na kuimarishwa, huku akisisitiza kuwa hatowaangusha katika utekelezaji wa majukumu yake.

Aidha, Hemed amewaahidi wanachama na wananchi kuwa ataendeleza mazuri yaliyofanywa na mlezi aliyemtangulia, akieleza kuwa dhamira yake ni kuona CCM inaendelea kukua na kuimarika mkoani humo.

Ameeleza kuwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2025–2030 umeendelea kujenga imani ya wananchi kwa chama hicho.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Stanslaus Nyongo, ameahidi kumpa ushirikiano mlezi huyo katika kipindi chote atakachohudumu mkoani humo.

Nyongo amesema mkoa huo unaendelea kupiga hatua za maendeleo na kuwataka wananchi kudumisha umoja na mshikamano, sambamba na kuunga mkono utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.

Naye Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kibaha, Dkt. Nicas Mawazo, amempongeza Makamu huyo wa Pili wa Rais kwa uteuzi wake na kuahidi kumpa ushirikiano katika kusimamia utekelezaji wa Ilani ya CCM na kuwahudumia wananchi.



Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...