Na Mwandishi Wetu, Mirerani

Mamia ya wakazi wa mji mdogo wa Mirerani, Wilaya ya Simanjiro, wamejitokeza katika mazishi ya marehemu Laura Lawrence Massawe, aliyekuwa mke wa Katibu wa Chama cha Wachimbaji Madini Mkoa wa Manyara (MAREMA), Tariq James Kibwe.

Mazishi hayo yalifanyika Mirerani, huku mwili wa marehemu ukizikwa katika eneo la Kia, Mkoa wa Kilimanjaro.

Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Kimadini wa Mirerani (RMO), George Kaseza, aliongoza waombolezaji katika mazishi hayo na kutoa pole kwa Kibwe pamoja na familia yote kutokana na msiba huo.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Madini Tanzania (FEMATA), Peter Kabepera, akimwakilisha Rais wa shirikisho hilo, John Bima, alitoa salamu za pole na rambirambi kwa familia ya marehemu.

Alisema Rais Bima hakuweza kuhudhuria mazishi hayo kutokana na kuwa nje ya nchi, hivyo kumtuma kumwakilisha katika msiba huo.

Naye Mwenyekiti wa MAREMA, Elisha Nelson Mnyawi, aliwapa pole wafiwa na kuwataka kuwa na moyo wa subira na kumtegemea Mungu katika kipindi hicho kigumu.

Viongozi wengine waliotoa pole ni pamoja na Mwenyekiti Mstaafu wa MAREMA, Justin Nyari, na Diwani wa Kata ya Mirerani, Salome Nelson Mnyawi, ambaye aliwataka watoto wa marehemu kuendelea kumpenda, kumheshimu na kumthamini baba yao katika kipindi hiki cha majonzi.

Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi mbalimbali, wadau wa sekta ya madini, ndugu, jamaa na wananchi wa maeneo mbalimbali.


Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...