Waziri wa Afya, Mhe. Mohamed Mchengerwa, leo tarehe 08 Novemba 2026, amefanya ziara ya kikazi ya katika Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila iliyopo jijini Dar es Salaam, kwa lengo la kukagua utoaji wa huduma za matibabu pamoja na kuzungumza na wagonjwa na watumishi wa afya.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mchengerwa amepongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa usimamizi mzuri wa hospitali na kwa ubora mkubwa wa huduma za kibingwa na kibobezi zinazotolewa kwa wananchi na kubainisha kuwa Muhimbili-Mloganzila imekuwa nguzo muhimu na ya kimkakati katika sekta ya matibabu nchini.

Pamoja na kutoa pongezi hizo, Waziri Mchengerwa ametumia fursa hiyo ya kipekee kuzungumza na wananchi waliofika kupata huduma.

Mhe. Mchengerwa amesisitiza kuwa lengo kuu la ziara hiyo ni kujadili kwa pamoja namna ya kuimarisha mifumo ya utendaji kazi na kujenga misingi thabiti ya uwajibikaji wa pamoja na kuongeza kuwa ni lazima kila mtumishi ahakikishe wagonjwa wanapata huduma bora, zenye hadhi na heshima bila kukumbana na vikwazo vyovyote visivyo vya lazima.

"Mifumo yetu ya utendaji kazi lazima iimarishwe ili kujenga misingi thabiti ya uwajibikaji. Tunataka wananchi wapate huduma bora na za heshima bila vikwazo," amesema Waziri Mchengerwa

Hatua hii ya Waziri inakuja wakati Wizara ya Afya ikiwa imedhamiria katika kutekeleza mikakati endelevu inayolenga kuhakikisha Taasisi zote za Afya za Umma nchini zinajenga imani kubwa kwa wananchi kupitia utoaji wa huduma zenye kiwango na hadhi ya kitaifa na kimataifa.

Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...