Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kupitia Ndaki ya Insia (College of Humanities) imeadhimisha miaka 40 ya elimu ya Akiolojia, katika hafla iliyofanyika leo tarehe 27 Novemba, 2026.

Akimuwakilisha Kamishna wa Uhifadhi Ngorongoro, Meneja wa Idara ya TEHAMA na Takwimu SACC Dkt. Aman Makota,  ameelezea umuhimu wa kutumia teknolojia katika kuhifadhi, kuandaa kumbukumbu na kutangaza urithi wa Taifa ili kurithisha elimu hiyo kwa kila kizazi. 

Dkt. Makota amesisitiza kuwa miaka 40 ya Akiolojia UDSM ni ushahidi wa mchango mkubwa wa chuo hicho katika kuelewa chimbuko la binadamu wa kale lililogunduliwa Ngorongoro, kujua historia ya Tanzania na dunia, pamoja na kuimarisha sekta ya utalii kupitia urithi.

“TEHAMA ina nafasi kubwa katika kuhifadhi taarifa za kiakiolojia, kurahisisha utafiti na kufikisha elimu ya urithi kwa vizazi vijavyo, Ngorongoro tutaendelea kushirikiana na UDSM, watafiti wengine kuhifadhi taarifa mbalimbali kisasa “ aliongeza Dkt Makota.

Kupitia Maadhimisho hayo wanafunzi na watafiti wamepata fursa ya kujifunza na kubadilishana uzoefu  sambamba kuongeza uelewa wa pamoja.

Ngorongoro imeshiriki kikamilifu maadhimisho hayo yenye kauli mbiu isemayo “Four Decades of Archaeology Education and Research: Heritage Preservation, Tourism and National Development” ambayo imewaleta pamoja wahadhiri, wanafunzi, watafiti na wadau wa makumbusho na uhifadhi nchini.














Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...