-Kampuni yapanga kupanua huduma na kuimarisha matumizi ya huduma za kidijitali ili kusaidia mawakala kukuza biashara zao

Mixx Tanzania inapanga kupanua huduma zinazopatikana kupitia mtandao wake wa mawakala zaidi ya 270,000 nchini, ili kuwaongezea fursa za kipato nje ya kamisheni wanazopata kutokana na miamala ya kuweka na kutoa fedha.

Mipango hiyo ni sehemu ya dhamira ya kampuni kuimarisha ushirikiano na mawakala wake kwa kupanua fursa za biashara, kuimarisha mawasiliano na kuongeza matumizi ya huduma za kidijitali katika shughuli zao za kila siku.

Akizungumza katika hafla ya ‘Mixx Wakala Brunch’ iliyofanyika Dar es Salaam leo iliyoadhimisha miaka 16 ya ushirikiano na mawakala, Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx Tanzania, Bw. Louis-Olivier Favot, alisema mtandao huo sasa unawahudumia Watanzania takribani milioni 28.

“Tangu enzi za Tigo Pesa hadi leo Mixx, ninyi ndio mmetusaidia kujenga biashara hii. Mnafungua biashara zenu mapema na kufunga usiku, mkiwahudumia wateja kila siku. Mnahakikisha fedha taslimu, salio na chenji vinapatikana, huku jamii ikiendelea kuwaamini,” alisema Favot.

Alisema kampuni inapanga kuongeza huduma katika vituo vya mawakala ili kupanua vyanzo vyao vya mapato na kuwawezesha kukidhi mahitaji zaidi ya kifedha ya wateja.

“Tunapanga kuongeza huduma kupitia vituo vyenu ili muweze kupata kipato, nje ya kamisheni za kuweka na kutoa fedha,” alisema.

Upatikanaji wa fedha taslimu na floti unaendelea kuwa muhimu katika shughuli za mawakala. Upungufu wake unaweza kuwazuia kukamilisha miamala, hivyo kuwakosesha kamisheni na kuwalazimu wateja kutafuta huduma katika vituo vingine.

Kupitia huduma ya Bustisha Wakala, iliyoanzishwa kwa kushirikiana na Benki ya KCB Tanzania, zaidi ya mawakala 7,000 tayari wanapata msaada wa kuongeza salio la kuendeshea biashara zao kila siku. Favot aliwahimiza mawakala wengi zaidi kutumia huduma hiyo ili kuimarisha uwezo wao wa kuwahudumia wateja.

Kampuni pia iliangazia App ya Mixx Wakala, inayowawezesha mawakala kusimamia miamala na kufuatilia mwenendo wa biashara zao kidigitali kupitia simu. Favot alisema Mixx itaendelea kuboresha huduma zake kwa kuzingatia maoni ya mawakala na kuwasaidia kunufaika zaidi na huduma zinazopatikana.

Katika mipango yake kuelekea mwaka 2030, Mixx inalenga kuwawezesha mawakala wengi zaidi kutumia zana za kidijitali kusimamia biashara zao na kuwahudumia wateja wengi zaidi.

Aidha, Favot alisema kutakuwa na mikutano ya mara kwa mara kati ya mawakala, yeye mwenyewe na timu ya uongozi wa kampuni. Mikutano hiyo itawapa mawakala nafasi ya kuwasilisha changamoto, kupendekeza maboresho na kujadili namna ya kuimarisha ushirikiano wao na Mixx.

Kampuni pia itakuwa ikipitia mara kwa mara masharti ya biashara na ushirikiano wake na mawakala ili kuhakikisha pande zote zinanufaika na juhudi za mawakala zinatambuliwa ipasavyo.

Favot aliwataka mawakala kuendelea kutoa maoni kuhusu uzoefu wao, changamoto wanazokutana nazo katika vituo vyao na huduma zinazohitajika na wateja, ili kusaidia kampuni kuboresha huduma zake.

Kwa upande wake, John Mkwizu, wakala wa Mixx anayefanya shughuli zake eneo la Magomeni, Dar es Salaam, alieleza umuhimu wa upatikanaji wa salio na matumizi ya zana za kidijitali katika biashara yake.

“Wateja wanatutegemea kupata fedha zao wanapozihitaji. Ninaposhindwa kukamilisha muamala, wanalazimika kutafuta wakala mwingine, nami ninakosa kamisheni. Upatikanaji wa salio la uwakala unaniwezesha kuendelea kuwahudumia, huku App ya Mixx Wakala ikinirahisishia usimamizi wa miamala yangu ya kila siku.

“Kama wakala, nataka kutoa huduma za kuaminika, kuwafanya wateja warudi tena na kupata kipato cha kutosha kukuza biashara yangu,” alisema Mkwizu.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mixx Tanzania, Louis-Olivier Favot, akizungumza na mawakala wa Mixx (hawapo pichani) wakati wa hafla ya Mixx Wakala Brunch iliyofanyika jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Hafla hiyo iliadhimisha miaka 16 ya ushirikiano na mawakala, ambapo kampuni ilitangaza mipango ya kupanua huduma kupitia mtandao wake wa mawakala zaidi ya 270,000 ili kuwaongezea fursa za kipato. Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Njia mbadala za Kidigitali na Usambazaji - Mixx Tanzania, Bw. Innocent Mosha.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...