-Ni yule anayemiliki mali za mabilioni ya fedha Tanzania na Kenya,DCEA yatoa kauli nzito
-Pia mbinu ya kutumia magari ya kifahari kusafirisha dawa za kulevya yabainika
Na Said Mwishehe,Michuzi TV
MTUHUMIWA wa dawa za kulevya ambaye ni Mtanzania anayeishi Mombasa nchini Kenya, Salehe Baseleman a.k.a Mbwiga anayenunua dawa za kulevya moja kwa moja kutoka nchini Afghanstan na kuzisafırisha katika nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania hatimaye amekamatwa na sasa anasubiri sheria ichukue mkondo wake
Inadaiwa Mbwiga amekuwa akisafirisha dawa za kulevya kwa njia ya bahari mpaka katika fukwe za Mombasa, nchini Kenya, kabla ya kuzisambaza katika nchi mbalimbali.
Mfanyabiashara huyo anaetuhumiwa na biashara ya dawa za kulevya ni miongoni kwa watuhumiwa saba waliokamatwa na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa Kulevya kupitia operesheni maalum iliyofanyika nchini.
Akizungumza leo Novemba 9,2026 jijini Dar es Salaam Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya(DCEA)Aretas Lyimo amesema baadhi ya watuhumiwa waliokamata ni vinara wa mtandao wa kimataifa wa usafrishaji na usambazaji wa dawa za kulevya wanaofanya shughui zao katika nchi mbalimbali, zikiwemo Afghanistan, Afrika Kusini, Msumbiji, Zambia, Malawi, Uganda, Kenya, Tanzania na Dubai.
“Mtuhumiwa huyu ambaye tunamshikilia pia anahusishwa na ukamataji wa dawa za kulevya tani 3.5 zilizokamatwa na DCEA
Desemba mwaka 2023 eneo la Kigamboni, jijini Dar es Salaam na mkoni Iringa.”
Akifafanua zaidi kuhusu operesheni iliyofanywa na Mamlaka hiyo amesema imewezesha pia kukamatwa jumla ya paketi 299 za dawa za kulevya, zikiwemo paketi 24 za heroin na paketi 275 za methamphetamine.
Kamishina Lyimo amesema dawa hizo zilikamatwa zikiwa zimefichwa ndani ya magari mawili aina ya Ford Ranger yenye namba za usajili T.950 ERA na T.417 EJZ, ambayo pia yanashikiliwa kutokana na kuhusishwa na uhalifu huo. watuhumiwa wanne (4) walikamatwa katika operesheni hiyo.
Amewataja watuhumiwa hao ni Juma Kisomeko(36), raia wa Uganda, dereva na mkazi wa Piji, nchini Uganda; Issa Nassoro(34), mfanyabiashara; Ibrahim Chembela(30), dereva; na Mohamed Shemtuu (45), dereva ambao hao ni wakazi wa Tabata, jjini Dar es Salaam.
“Baada ya kukamatwa na kuhojiwa, watuhumiwa hao wameeleza kuwa, dawa hızo walizichukua Mombasa, Kenya na kuzisafirisha kuingia Tanzania kupitia mpaka wa Horohoro mkoani Tanga.
“Kutokana na maelezo hayo, Mamlaka iliwasiliana na mamlaka husika nchini Kenya na kushirikiana kiutendaji kwa lengo la kubaini chanzo, eneo lililotumika kuhifadhi dawa hizo, pamoja na kuwabaini wahusika wengine wa mandao huo.”
Akieleza zaidi amesema kupitia ushirikiano huo, Novemba 7,2026, DCEA na Kitengo cha Kitaifa cha Kudhibiti Dawa za Kulevya chini Kenya (NANB) zilfanikisha ukamataji wa paketi 454 za dawa ya kulevya aina ya methamphetamine kutokana na operesheni liyoranyıka eneo la Kwale jini Mombasa, Kenya.
Katika operesheni hiyo, watuhumiwa wengine watatu walikamatwa. Watuhumiwa hao ni Salehe Baseleman maarufu Mbwiga ambaye ni raia wa Tanzania, mfanyabiashara na mkazi wa Mombasa, nchini Kenya.Seif Hamadi maarufu Babu Seif ambaye ni raia wa Tanzania, mvuvi na mkazi wa Kinondo, Mombasa, chini Kenya na Zuraicah Hussein ambaye ni raia wa Uganda, mfanyabiashara na mkazi wa Shirazi, Mombasa, nchini Kenya.
“Taratibu za kisheria kati ya Tanzania na Kenya zinaendelea ili kuhakikisha watuhumiwa wote wanafikishwa mbele ya vyombo vya sheria kwa hatua zaidi.Mafanikio yaliyopatikana katika operesheni hii yanaonesha umuhimu wa ushirikiano wa kitaifa, kikanda na kimataita katika kukabillana na dawa za kulevya Duniani.
“Hivyo, Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inatoa mwito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa kuhusu viashiria vya uwepo wa biashara na matumizi ya dawa za kulevya,”amesema Kamishina Jenerali Lyimo.

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...