Ngorongoro imeendelea kung’ara katika ramani ya utalii wa kimataifa baada ya wageni kutoka Safari Club International ya Marekani, pamoja na washiriki kutoka Afrika Kusini, Msumbiji, Malawi na Uganda, kuvutiwa na maajabu ya eneo hilo na kuahidi kuwa mabalozi wa utalii wa Tanzania katika mataifa wanayotoka.
Wageni hao waliduwazwa na maajabu ya Ngorongoro ikiwa ba pamoja na kushuhudia wanyama wakubwa watano Big Five, na makundi ya Pundamilia, Nyati, Nyumbu, swalabna nyani wakifurahia maisha Ngorongoro ambayo ni kivutio bora cha utalii Afrika.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mkurugenzi Msaidizi kutoka Idara ya wanyamapori, Wizara ya Maliasili na Utalii, amesema ziara hiyo ni sehemu ya juhudi za Serikali katika kuitangaza Tanzania kimataifa na kuunga mkono kampeni ya The Royal Tour inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Ziara hii imethibitisha msemo wa wahenga usemao Mwenda tezi na omo marejeo ngamani Kwani Hifadhi hii imeendelea kuwa daraja la kuitangaza Tanzania kupitia uzoefu halisi wa wageni, ambapo kila anayefika Ngorongoro hupata uhalisia wa ndoto yake kwa kushuhudia maajabu ya wanyamapori, malikale na urithi wa utamaduni, maporomoko ya maji, mchanga unaohama, kasoko za Ngorongoro, Empakai na Olmoti.



.jpeg)


.jpeg)


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...