-Asisitiza huduma bora kwa Watanzania wote
WAZIRI MKUU, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka viongozi na watendaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kudumisha ushirikiano na maelewano katika kutekeleza majukumu yao, akisisitiza kuwa migogoro baina yao inakwamisha utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Jumatatu, Novemba 16, 2026) wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 40 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) katika ukumbi wa Kwatunza jijini Mwanza, akieleza kuwa Wabunge, Madiwani, Mameya, Wenyeviti wa Halmashauri na Wakurugenzi Watendaji wana wajibu wa kufanya kazi kwa pamoja badala ya kutumia nguvu na muda mwingi katika migogoro isiyo na tija kwa Watanzania.
“Viongozi wote katika Mamlaka za Serikali za Mitaa watumikieni wananchi na acheni migongano baina yenu, nimeona jambo la Kibaha, kweli jambo lile linapaswa kufanywa na viongozi wa ngazi ya wilaya?, hapana."
"Na isivyobahati, nchi nzima imeona lile jambo wakati kwenye kikao hicho hicho pengine kulikuwa na mambo ya msingi yanayowahusu wananchi yaliyojadiliwa lakini hakuna anayefahamu, kwa sababu gani?, jambo lisilo na tija limefunika yote,” amesema Waziri Mkuu.
Amesema Serikali inatambua na kuthamini mchango wa ALAT katika kuunganisha na kuwakilisha Mamlaka za Serikali za Mitaa, hivyo Jumuiya hiyo inapaswa kuendelea kuwa daraja imara kati ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa.
Waziri Mkuu ameeleza kuwa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa ni sehemu ya mfumo mmoja wa utawala wenye dhamira ya kuwahudumia wananchi, hivyo kuimarisha ushirikiano kutasaidia kuongeza ufanisi wa utoaji huduma za msingi kwa jamii.
"Kwa muda mrefu, kumekuwa na utaratibu usio rasmi, kwamba Serikali Kuu ni kama ina watu wake inaowahudumia, ukija Serikali za Mitaa nako ni kama wanao aina fulani tu ya watu inaowahudumia, hapana, Watanzania ni wetu sote, tuwahudumie ipasavyo na kwa mujibu wa taratibu zilizopo," amehimiza Dkt. Mwigulu.
Aidha, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kutoa vibali vya ajira ili kukidhi mahitaji ya watumishi katika kada mbalimbali. "Katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali iliidhinisha nafasi 41,500 za ajira mpya, huku katika mwaka wa fedha 2026/2027 ikipanga kutoa nafasi 52,124, zikiwemo 45,000 za ajira mpya na 7,124 za ajira mbadala."
"Pia, bajeti ya matumizi ya kawaida kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa imeongezeka kutoka shilingi bilioni 157.57 mwaka 2021/2022 hadi shilingi bilioni 365.28 mwaka 2026/2027. Hatua hizi zinalenga kuhakikisha wananchi tunaowahudumia wanapata huduma bora," amesisitiza Waziri Mkuu.
Mkutano Mkuu wa 40 wa ALAT Taifa umefanyika chini ya kaulimbiu isemayo “Ongeza Ufanisi wa Utoaji wa Huduma za Msingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili Kufikia Malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.”
Dkt. Mwigulu ameihakikishia ALAT kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuzijengea uwezo na kuweka mazingira wezeshi ya utekelezaji wa majukumu yao ili kuharakisha maendeleo ya Taifa.
Awali akimkaribisha Waziri Mkuu, Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amewataka viongozi wa ALAT na viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na uwajibikaji huku wakitanguliza maslahi ya umma ili wananchi waone tija ya taasisi zao.

.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

.jpeg)

.jpeg)
.jpeg)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...