Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, ameeleza nia ya kuitisha kikao kitakachowakutanisha viongozi wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) na wawakilishi wa taasisi za fedha, kwa lengo la kutafuta suluhisho la muda mrefu la changamoto za kifedha zinazowakabili wahariri nchini.
Akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Mwaka wa TEF uliofanyika mkoani Morogoro, Dkt. Nchemba aliitaja Benki ya NMB katika maelezo yake kuhusu umuhimu wa ushirikiano na taasisi za fedha katika kuimarisha ustawi wa kifedha wa wadau wa sekta ya habari.
Katika mkutano huo, Waziri Mkuu aliikabidhi NMB cheti cha kutambua mchango wake katika kufanikisha mkutano huo kupitia udhamini wake. Cheti hicho kilipokelewa na Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya NMB, Janeth Shango, kwa niaba ya benki.
NMB inaendelea kuthamini mchango wa vyombo vya habari katika maendeleo ya Taifa na kuimarisha ushirikiano na wadau wa sekta hiyo, sambamba na dhamira yake ya kupanua fursa za upatikanaji wa huduma za kifedha zinazochangia ustawi wa jamii.
#NMBKaribuYako #TEF2026


.jpeg)
.jpeg)

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...