Shirika la Posta Tanzania (TPC) limeendelea kuimarisha nafasi yake katika sekta ya usafirishaji na usambazaji wa bidhaa nchini kupitia ushiriki wake katika uzinduzi wa jukwaa la biashara la Xerin Market, linalolenga kuwaunganisha wafanyabiashara na wateja kupitia teknolojia pamoja na huduma za usafirishaji.

Uzinduzi huo umefanyika Novemba 11, 2026, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, ukihudhuriwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade), Ephraim Mafuru, aliyemwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara, pamoja na Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Posta, Ferdinand Kabyemela, aliyemwakilisha Postamasta Mkuu.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kabyemela amesema mafanikio ya biashara za mtandaoni hayaishii katika kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi kupitia teknolojia pekee, bali yanahitaji pia mfumo madhubuti wa usafirishaji na usambazaji wa bidhaa, ambao Posta imejipanga kuutoa.

Amesema ushirikiano huo utaongeza fursa kwa wafanyabiashara wa Kariakoo na maeneo mengine nchini kufikia masoko mapana zaidi, huku wateja wakinufaika na huduma za usafirishaji na usambazaji wa bidhaa.

Kupitia ushirikiano huo, Posta Tanzania inaendelea kutumia mtandao na miundombinu yake kuunganisha biashara, watu na fursa za kiuchumi katika maeneo mbalimbali nchini.










Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...