Na Farida Mangube, Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Queen Sendiga, amezindua namba maalumu ya simu itakayowawezesha wananchi kuwasilisha kero, changamoto na maoni yao ili zipatiwe ufumbuzi kwa haraka.

Uzinduzi huo umefanyika Novemba 9, 2026, katika Ukumbi wa Mikutano wa Magadu, Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Sendiga amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada za Serikali za kuhakikisha changamoto za wananchi zinashughulikiwa kwa wakati, akisisitiza umuhimu wa kuzitafutia ufumbuzi kwa haraka.

Amesema wananchi watatumia namba 0800114045 kuwasilisha kero zao bila malipo, huku gharama za huduma hiyo zikigharamiwa na Serikali.






Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...