SHIRIKA la Room to Read, limeingia makubaliano na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ikiwa ni sehemu ya kuendeleza, kuimarisha na kupanua ushirikiano eneo la uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana, hususan wasichana.
Akizungumza
katiha hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkazi wa Room to Read, Bi. Joan Ndaambuyo Minja alisema
wanatambua na kuthamini
dhamira ya Serikali ya kuhakikisha kila mtoto anapata elimu bora, jumuishi na
yenye kumjengea maarifa, stadi na uwezo wa kushiriki katika maendeleo ya Taifa,
hivyo lina kila sababu ya kuunga mkono juhudi hizo.
Alisema
shirika hilo linauchukulia
ushirikiano na Serikali kuwa ni sehemu ya kutekeleza vipaumbele vya kitaifa
katika sekta ya elimu, badala ya kuwa utekelezaji wa programu za Room to Read
moja kwa moja.
“…Leo
ni siku muhimu katika historia ya ushirikiano kati ya Taasisi ya Elimu Tanzania
na Shirika la Room to Read Tanzania. Utiaji saini wa Hati hii ya Makubaliano
unaweka msingi rasmi wa kuendeleza, kuimarisha na kupanua ushirikiano wetu
katika maeneo mawili muhimu: uimarishaji wa stadi za kusoma na kuandika kwa
watoto, pamoja na kukuza stadi za maisha na usawa wa kijinsia kwa vijana,
hususan wasichana,” alisema, Bi. Minja.
Alibainisha kuwa makubaliano waliosaini yanaendana na mwelekeo wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014, Toleo la 2023, inayosisitiza umuhimu wa elimu yenye ubora, usawa wa
fursa, ujumuishi na ushirikishwaji wa wadau mbalimbali katika kuendeleza elimu
nchini.
Aliongeza kuwa Sera inatambua kuwa jukumu la
kuboresha elimu si la Serikali pekee. Linahitaji ushirikiano wa karibu kati ya
Serikali, taasisi zake, sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, wadau wa
maendeleo, wazazi na jamii kwa ujumla.
“…ushirikiano huu
unaendana na matarajio ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga
kujenga Taifa lenye watu wenye maarifa, ujuzi, ubunifu na uwezo wa kukabiliana
na mabadiliko ya kiuchumi na kijamii. Dira hii inatukumbusha umuhimu wa
kuwekeza katika rasilimali watu kuanzia hatua za awali za ujifunzaji,
kuimarisha elimu yenye ubora na kuhakikisha kuwa wanawake na wanaume, wasichana
na wavulana wanapata fursa sawa za kujifunza, kuendeleza vipaji vyao na kushiriki
katika maendeleo ya Taifa,” amesisitiza, Bi. Joan Minja.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba akizungumza katika hafla hiyo, alisema miongoni mwa malengo makuu ya Hati ya Makubaliano waliosaini ni Kushirikiana katika uandaaji, kupitia na kuhuisha vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili viendane na viwango vya Mitaala ya Taifa, kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014, Toleo la 2023, na Mwongozo wa Kitaifa wa Mitaala ya ElimuMsingi, kwa lengo la kuimarisha ubora na ufanisi wa ujifunzaji wa stadi za msingi.
Alisema mengine muhimu waliokubaliana na katika
ushirikiano huo ni, kuimarisha umahiri wa walimu kupitia mifumo ya mafunzo ya
ualimu kabla ya kuanza kazi na mafunzo endelevu kwa walimu walio kazini, kwa
kuandaa na kutekeleza mafunzo kwa kuzingatia Mkakati wa Taifa wa Maendeleo na
Usimamizi wa Walimu pamoja na vipaumbele vya kitaifa vya kuimarisha umahiri wa
walimu na kuboresha ufundishaji na ujifunzaji darasani.
Aidha alibainisha na
Pia tumekubaliana; kuwezesha upatikanaji wa elimu bora kwa usawa na bila ubaguzi,
kwa kuzingatia mahitaji ya kijinsia, kwa mujibu wa Mkakati wa Taifa wa
Maendeleo ya Jinsia pamoja na vipaumbele vya elimu jumuishi vilivyoainishwa.
| Picha ya pamoja. |



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...