Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha

Wafanyakazi wa viwandani wametakiwa kuhakikisha wanaelewa masharti yote ya mikataba ya ajira kabla ya kuisaini ili kuepuka migogoro na changamoto zinazoweza kujitokeza katika uhusiano wao na waajiri.

Ushauri huo umetolewa Novemba 6, 2026 na Timu ya Wataalamu wa Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia (Samia Legal Aid), Manispaa ya Kibaha, iliyofika katika viwanda mbalimbali vilivyopo Kata ya Misugusugu, Mkoa wa Pwani.

Ziara hiyo imelenga kuwajengea wafanyakazi uelewa kuhusu haki na wajibu wao kwa mujibu wa sheria, hususan katika masuala yanayohusu mikataba ya ajira.

Katika kampeni hiyo, wafanyakazi wamepatiwa elimu kuhusu mambo muhimu ya kuzingatia kabla ya kuingia mikataba ya ajira, huku wakipewa nafasi ya kuuliza maswali na kueleza changamoto wanazokutana nazo katika utekelezaji wa mikataba hiyo.

Wataalamu wa sheria walitoa ufafanuzi kuhusu masuala mbalimbali yaliyoulizwa na wafanyakazi, kwa lengo la kuwasaidia kuelewa haki zao na wajibu wao katika mazingira ya kazi.

Kampeni hiyo ni sehemu ya jitihada za kuifikisha huduma ya msaada wa kisheria kwa wananchi katika maeneo yao, wakiwemo wafanyakazi wa sekta mbalimbali.







Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...