Serikali imeitaka Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kuimarisha majadiliano ya pamoja kati ya waajiri na wafanyakazi ili kupunguza migogoro isiyo ya lazima na kujenga mazingira bora ya kazi nchini.

Wito huo umetolewa Novemba 23, 2026, na Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi Tanzania Bara, Vallensi Wambali, kwa niaba ya Kamishna wa Kazi, Suzan W. Mkangwa, wakati akifungua Baraza Kuu la TUCTA lililofanyika katika Ukumbi wa Royal Village jijini Dodoma, ambapo amesisitiza kuwa majadiliano yanapaswa kuwa njia ya kutafuta suluhu na maelewano badala ya kuwa chanzo cha ushindani na migogoro kati ya pande hizo.

Amesema Serikali inatambua umuhimu wa vyama vya wafanyakazi katika kulinda haki na maslahi ya wanachama wao, huku akibainisha kuwa Tanzania imeridhia mikataba nane ya msingi ya Shirika la Kazi Duniani (ILO), ikiwemo Mkataba Na. 98 unaohusu haki ya kujipanga na majadiliano ya pamoja. Aidha, amevitaka vyama hivyo kutumia uhuru viliopewa kwa uwajibikaji na kuendelea kutoa elimu ya sheria za kazi kwa wanachama wao kuhusu haki na wajibu wao.

Wambali amesisitiza pia umuhimu wa waajiri na wafanyakazi kutumia mifumo ya ndani kutatua changamoto zinazojitokeza na pale zinaposhindikana kuziwasilisha katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) pamoja na vyombo vingine vya kisheria, akieleza kuwa ushirikiano kati ya Serikali, waajiri na wafanyakazi ni msingi wa kulinda haki, kuongeza tija na kuchochea ukuaji wa uchumi wa Taifa.

Kwa upande wake, Wakili Noel Nchimbi Mwenyekiti wa bodi ya Wadhamini TUCTA, amesema mkutano huo ni halali kwa mujibu wa akidi iliyopo, na kimsingi uchaguzi utafanyika kuanzia tarehe 25 na 26 Novemba 2026, kufuatia upngozi wa TUCTA kuisha muda wake tangu tarehe 13 Novemba, hivyo matarajio ni kupata viongozi bora watakao rudisha mahusiano bora mahali pa kazi kwa kuzingatia umoja na mshikamano.

Akizungumza Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TUCTA 2026, Aloysius Mapembe, amesema uchaguzi wa Shirikisho hilo utafanyika kwa tarehe iliyopangwa kwa mujibu wa Katiba ya TUCTA, akiwatoa hofu wafanyakazi kuhusu maandalizi ya uchaguzi huo, amesema maandalizi yanaendelea na kuvihakikishia vyama vyote vinavyostahili kushiriki kuwa taratibu za uchaguzi zinafuatwa kwa kuzingatia Katiba, huku akiwataka wafanyakazi kujitokeza kushiriki.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...