Serikali kupitia Ofisi ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu -TAMISEMI imezitaka Wilaya ya Ilala, Temeke , Kinondoni pamoja na Mafia kuweke mifumo madhubuti wa uratibu uwajibikaji na ufuatiliaji wa mipango mkakati ya usimamizi wa taka za Plastiki jambo ambalo litaleta na tija kwa taifa katika kulinda mazingira na kuweka msingi wa mabadiliko ya kweli na kutengeneza fursa za kiuchumi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akizindua mipango mkakati ya kuboresha Usimamizi WA Taka za Plastiki Wilaya ya Ilala, Temeke, Mafia na Kinondoni, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – TAMISEMI anayeshughulikia Miundombinu Mhandisi Rogatus Mativila, amesisitiza umuhimu wa vikao vya menejimenti na kamati za halmashauri kuhakikisha ufuatiliaji endelevu pamoja na kujadili utekelezaji wake.
Mwenyekiti wa Bodi ya Mtandao wa Mashirika ya Kiraia yanayoshughulikia Mabadiliko ya Tabianchi Tanzania (FORUMCC - Forum CC) Yusta Kibona, meiomba serikali kutoa muongozo Kwa Halmashauri ili vipaombele vya mkakati hiyo viingizwe katika mipango ya maendeleo na bajeti kila mwaka.
Mwakilishi wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Elias Chundu, amesisitiza umuhimu wa wadau kushirikiana katika kulinda mazingira, kuwepo kwa sheria rafiki na kuimarisha utekelezaji wa mipango ya kupunguza uzalishaji wa taka ngumu.
Kwa upande wao Wawakilishi wa halmashauri hizo wameahidi kutekeleza kwa vitendo mikakati iliyowekwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha malengo ya usimamizi bora wa taka za plastiki yanafikiwa.
Katika hafla hiyo, wametoa Tuzo kwa masoko waliofanya vizuri katika usimamizi wa mazingira, ikiwa ni sehemu ya kuwahamasisha kuendeleza juhudi za kutunza mazingira.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...