Na Mwandishi Wetu – Mwanza

SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imeendelea kuweka mazingira wezeshi kwa watu wenye ulemavu kupata fursa za ajira, ambapo katika kipindi cha miaka mitano ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, zaidi ya watu wenye ulemavu 1,411 wamepata ajira katika maeneo mbalimbali nchini.

Akizungumza na watu wenye ulemavu na wadau mbalimbali, Naibu Katibu kutoka Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Mhandisi Samweli Tanguye, amesema mafanikio hayo yanaonesha hatua ambazo Serikali imeendelea kuchukua katika kuhakikisha watu wenye ulemavu wanashirikishwa na kunufaika na fursa za ajira na maendeleo.

Mhandisi Tanguye amesema watu wenye ulemavu wanapaswa kutumia fursa zinazopatikana kwa kujitokeza na kufuatilia taarifa sahihi za ajira kupitia vyanzo rasmi, huku akisisitiza umuhimu wa kujiweka kwenye mifumo inayotumika katika mchakato wa ajira ili kuongeza uwezekano wa kunufaika na fursa hizo.

Aidha, ametoa angalizo kwa watu wenye ulemavu kuwa makini na taarifa za ajira zinazotolewa na watu au vyanzo visivyo rasmi, akisisitiza kuwa waombaji wanapaswa kuhakiki taarifa na kufuata njia rasmi ili kuepuka utapeli na kupoteza fedha kwa watu wanaodai kuwa wanaweza kuwapatia ajira.

Pia, amesisitiza umuhimu wa kuendelea kuwabaini na kuwaibua watu wenye ulemavu ambao bado wamefichwa au hawajafikiwa na taarifa za fursa za ajira, ili waweze kutambua fursa zilizopo, kuomba ajira na kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya Taifa.

Maadhimisho ya Wiki ya Kitaifa ya Watu Wenye Ulemavu yanaendelea jijini Mwanza ambapo mada mbalimbali zinazohusu mustakabali wa wenye ulemavu zinawasilishwa katika makongamano kuelekea kilele cha Siku ya Watu wenye Ulemavu Duniani tarehe 03 Desemba, 2026, yakiwa na kaulimbiu isemayo ”Sauti Zetu, Maoni Yetu, Mustakabali Wetu,”ambayo inasisitiza umuhimu wa kusikiliza sauti za watu wenye ulemavu, kuzingatia maoni yao na kuhakikisha wanakuwa sehemu ya kujenga mustakabali wa Taifa.





Next
This is the most recent post.
Previous
Older Post

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...